Katika kuelekea kilele cha maadhimisho ya siku ya wanawake duniani Ofisi ya maendeleo ya jamii Manispaa ya Lindi ikishirikiana na ofisi ya Mkurugenzi,kamati ya dawati la kijinsia(TPF-NET LINDI),Wambunge wa majimbo yote Lindi mjini na Mchinga pamoja na wadau mbalimbali watoa bati 25 kwa Bi. Bibie Ally Bakari Nakulama mkazi wa Mtaa wa Ruaha Kata ya Mnazimmoja ambaye alipata ajali ya nyumba yake kudondokewa na mbuyu na kupoteza mtoto mmoja huku yeye na binti yake kujeruhiwa vibaya.
Kamati ya Dawati la kijinsia polisi(TPF-NET LINDI)wakitoa mchango wao wa bati kwa mhanga wa ajali.
Bi.Bibie Ally Bakari Nakulama akipokea risiti ya manunuzi ya bati kutoka kwa Diwani viti Maalum kata ya Mnazimmoja.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa