Uwepo wa bahari ya Lindi ambayo huchukua eneo la kilomita 112 za mraba za eneo la Manispaa ni fursa kubwa kwa kuvutia wageni na shughuli za kiuchumi kama uvuvi, usafirishaji, uzalishaji wa gesi na mafuta na chumvi. Shughuli hizi bado hazijachangia kwa kiasi kikubwa katika uchumi wa wananchi wa Manispaa ya Lindi kutokana na uwezo mdogo wa uendeshaji wa shughuli hizo pamoja na uwekezaji mdogo katika maeneo hayo. Pia kuna uwanda wa misitu asilia ambayo ni fursa ya uwekezaji kwa mazao mbalimbali yatokanayo na misitu. Halmashauri ya Manispaa kupitia mpango mkakati wake itaboresha mazingira ya uwekezaji ili kuweza kuwavutia wawekezaji katika fursa zake zilizopo.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa