Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ikiongozwa na Mkuu wa Wilaya Ndugu Shaibu Ndemanga imeandaa maombi maalum katika miaka 60 ya Uhuru ikiambatana na maombi kwa ajili ya kupata mvua.Maombi hayo yamefanyika leo tarehe 28/11/2021 katika ukumbi wa St.Andrea Kagwa ambapo mgeni rasmi ni Mkuu wa Mkoa Mh.Zainab Telack.
Viongozi mbalimbali wakiwemo Katibu Tawala Mh.Rehema Madenge,Mbunge wa jimbo la Lindi mjini Mh.Hamida Abdallah,Mstahiki Meya Mh.Frank Magali,Katibu Tawala wa Wilaya Ndugu Thomas Safari na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Ndugu Juma Mnwele wamehudhuria maombi hayo.
Tukio hilo limeongozwa na viongozi wote wa dini wa madhehebu mbalimbali wakisindikizwa na waumini wao.Miongoni mwa viongozi hao ni pamoja na Sheikh wa Mkoa lakini pia Mchungaji Christopher Mwakasege alikuwepo kwa ajili ya kushiriki maombi hayo maalum baada ya kupata mwaliko kutoka kwa Mkuu wa Wilaya.
Mbali na maombi hayo tukio la maombi lilienda sambamba na shughuli za utoaji wa chanjo ya UVIKO-19 na uchangiaji damu ambapo wanafunzi na wananchi wamejitokeza kuchangia damu na kupata chanjo ya UVIKO-19.
Aidha Bi. Zainab Telack amewashukuru viongozi na wananchi wote walioshiriki maombi hayo ambapo amewaasa kuomba Mungu juu ya kuliombea Taifa na kizazi chetu.Amesema“Mimi ninawashukuru wananchi wa Lindi kwa kuitikia wito wetu na kukubali kuja ili kwa pamoja tuweze kumuomba Mungu kwa yale ambayo tunatarajia kumuomba mimi nawashukuru sana”
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255717469888
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa