• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

Utalii

Manispaa ya Lindi ni Mji mdogo wenye nyumba kadhaa za wageni, migahawa na hoteli. Mji unapendeza sana. Shukrani kwa kipindi cha ukoloni kwani kuna idadi ya majengo ya kupendeza.

  • Makao Makuu ya zamani ya Utawala wa Jeshi la Uingereza
  • BOMA, na tini zake za kunyonga zinazokua katika fursa za utalii.
  • Fukwe nzuri kwenye pwani ya Bahari ya Hindi pia huvutia watalii.
  • Kisiwa cha Popo (Kisiwa cha Popo), ambapo popo  hupumzika wakati wa mchana, hufanya utalii mzuri wa kusafiri katika Manispaa.

Changamoto kuu iliyokuwa inaikumba sekta ya utalii ilikuwa ni ukosefu wa uhusiano mzuri na maeneo mengine, kufika Manispaa ya Lindi hapo zamani ilikuwa ngumu. Lakini miundombinu ya leo inatoa uhusiano mzuri kati ya mikoa ya Mashariki na Kusini. Ujenzi wa barabara nzuri, ya lami kwenda Dar es Salaam, na barabara kutoka Daraja la Rufiji hadi Mingoyo, imeboresha hali hiyo imepelekea  kufupisha muda wa kusafiri hadi saa tano au sita. Kadiri watalii wanavyozidi kugundua uzuri wa pwani ya Kusini mwa Tanzania, kuna uwezekano wa kufanikiwa kwa uwekezaji katika huduma kwa watalii.


VIVUTIO VYA KITALII KATIKA MANISPAA YA LINDI

Vivutio vya utalii vipo katika sehemu tatu:

  • Vivutio vya utalii
  • Vivutio vya Malikale(kihistoria)
  • Vivutio vya Utamaduni(urithi wa utamaduni)

A. VIVUTIO VYA UTALII

S/N
KIVUTIO
MAELEZO
PICHA
1
Mjusi Mkubwa duniani
Eneo la Tendaguru ndipo yalipogunduliwa mabaki ya mijusi ya kale (Dinasours) mnamo mwaka 1908 na Injinia wa Kijerumani aitwaye B. Sattler alipokuwa anafanya utafiti wake wa Sayansi ya miamba.Baada ya kuripoti mabaki hayo kwa wanasayansi wa mambo ya kale huko Berlin, nchini Ujerumani, Taassisi na Makumbusho ya Malikale ya Ujerumani ilileta wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti katika eneo hilo. Utafiti ulifanyika kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 1909-1913 na mabaki ya mijusi yaliyopatikana yalisafirishwa hadi Ujerumani. 


Picha ya Mjusi
Eneo la Tendaguru
2
Fukwe za bahari
Manispaa ya Lindi ina eneo kubwa la Fukwe za bahari zaidi ya Kilometa 120.Maeneo hayo ni kivutio kikubwa kwa watalii kutokana na uwepo wa Matumbawe (Coral reefs) na shughuli mbalimbali kama uvuvi.

Eneo la fukwe ya bahari

Matumbawe
3
Mapango ya Kitumbikwela
Mapango ya Kitumbikwela, yaliyotumiwa kama maficho wakati wa vita, mafichio ya mali pamoja na vitu vya thamani. Inasemekana mapango haya yalitumiwa na Wajerumani kama sehemu ya maficho katika kipindi cha vita kuu ya kwanza ya dunia (1914-1918).


Mapango ya Kitumbikwela
4
Misitu ya hifadhi
Katika eneo la Manispaa ya Lindi wapo baadhi ya wanyamapori hususani katika Misitu ya hifadhi.Wanyama kama vile Tembo, aina mbalimbali za Nyoka, Simba,Mamba, na wengine wengi huonekana katika hifadhi hizo.Misitu ya Hifadhi iliyopo Manispaa ya Lindi ni pamoja na Msitu wa Dimba (Kata ya Kilolambwani na Mvuleni),Msitu wa Likipo na Noto (Kata ya Tandangongoro).Pia baadhi ya wanyama hupatikana katika eneo la hifadhi ya Selous ambayo ipo kata ya Milola na Rutamba.



5
Misitu ya hifadhi ya mikoko
Mikoko ni aina ya miti au vichaka vinavyopatikana katika zaidi ya nusu ya fukwe za bahari za maeneo ya kitropiki ulimwenguni. Kuna jamii mbalimbali za mikoko. Kwa kawaida,miti hiyo hukua katika sehemu za fukwe zilizo na mchanganyiko wa maji ya bahari na maji baridi katika maeneo ambako mikondo yenye nguvu hukutana na ile isiyo na nguvu. Ingawa mimea mingi haiwezi kukua katika maji hayo yenye chumvi nyingi, mikoko hukua huko kwa urahisi.Katika Manispaa ya Lindi misitu ya hifadhi ya mikoko hupatikana pembezoni ya bahari ya Hindi.



B. VIVUTIO VYA MALIKALE

S/N
KIVUTIO
MAELEZO
PICHA
1
Majengo ya kihistoria
Jengo la kale (Gofu) katika kata ya Mikumbi lilijengwa na Waarabu katika kipindi cha Utawala wa Sultan wa Omani Zanzibar ambaye ni Sultan Sayyid Said ambae baada ya kuhamishia makao makuu yake Zanzibar kutoka Omani mnamo mwaka 1840.


2
Jengo hili lilojengwa na Waarabu katika karne ya 13 na 14 (miaka ya 1200 na 1300), Jengo hili lina linaonesha lilikuwa linatumika kwa shughuli za kibiashara na makazi ya Wafanya biashara.


3
Hili ni jengo la kale lililopo eneo la kikwetu, jengo hili kihistoria lilikuwa ni jengo mojawapo katika majengo kadhaa ya Walowezi wa Kijerumani ambao walianzisha mashamba ya Katani katika eneo hili la Kikwetu. Eneo hili lilikuwa ndio makazi yao ambapo kuna Majengo yanayozidi manne ambapo mawili katika hayo bado yapo na yanamuonekano kama huo katika picha. Jengo hili lilijengwa kipindi cha Utawala wa Wajerumani Tanganyika (1880-1918) na baadae (baada ya vita kuu ya kwanza ya Dunia 1914-1918) jengo hili lilichukuliwa na Waingereza. Eneo hili lilikuwa ni Shamba la katani lenye hekari 16000. Jengo hili lina sehemu kuu tatu ambazo ni eneo la juu ya nyumba (hiko kighorofa cha juu), sehemu ya chini (yaani ground floor) na sehemu ya chini ya ardhi (underground floor).

4

Muonekana wa njia ya kwenda chini kuifikia sehemu ya ardhini (underground floor). Njia hii kwa nje ni ndogo na inaupana mkubwa kwa ndani kiasi cha kuweza kusimama na kutembea. Njia hii ilijengwa kwa mtindo huo makusudi kwa lengo la kiusalama zaidi ambapo kama Adui anafika hawezi kutambua kama ni njia. Njia hii inakupeleka katika underground floor ambapo nayo imejengwa kama nyumba ya makazi.


5
Hii ni moja ya sehemu ya ndani inayopatikana katika ground floor ya Jengo hili. Sehemu hii ilitengwa mahsusi kwaajili ya mchezo wa pool pekee, ambapo hiyo meza na mipira yake pamoja na fimbo za kuchezea huo mchezo vipo mpaka sasa hivi.chumba hiki kinaonesha kilikuwa ni kwa mchezo huo tu kutokana na uwepo wa meza ya mchezo huo pamoja na kete na fimbo zake. Utawala wa Wajerumani Tanganyika walianzisha Mchezo  wa Pool table  mnamo (1880-1918) katika kata ya Rasbula ,mtaa wa Kikwetu.

6
Jengo hili ni gereza la wafungwa watumwa ambao ni waswahili.Limejengwa karne ya 13 hadi 15 na utawala wa Waarabu.


7
Msikiti wa Bomolea
Msikiti wa Bomolea unaopatikana katika kata ya Mitandi Lindi Mjini. Msikiti huu unaonesha athari na alama za uwepo wa Waarabu katika eneo hili. Msikiti huu juu yake una Kuba hilo linaloonekana pichani ambalo ni la zamani na lipo tofauti na hilo jingo hapo chini. Kimsingi aina hiyo ya ujenzi ni aina ya kale ya ujenzi hasa kwenye misikiti iliyojengwa na Waarabu katika kipindi hiko.

8
Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Edward Steer
Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Edward Steer Lindi ambalo ni uthibitisho wa ujio wa Wamsionari katika Manispaa ya Lindi (Lindi Mjini) ambalo lilijengwa na Wamisionari katika harakati zao za kueneza dini ya ukristo katika ukanda wa Kusini. Kanisa hili kihistoria lilitembelewa na ST. Edward Steer mnamo tarehe 18 Oktoba mwaka 1876.

9
Mnara wa kihistoria
Mnara unaonesha historia ya miaka 100 ya Ukristu katika Manispaa ya Lindi (Lindi Mjini).Mnara huu unaonesha baadhi ya Wamisionari ambao walioendesha Misa ya kwanza katika Manispaa ya Lindi mnamo tarehe 03-12-1894.



10
Kaburi la sharifu
Kaburi la sharifu katika eneo la Bomolea, hili ni moja ya kaburi katika makaburi ya masharifu wengi waliowahi kuishi katika Manispaa ya Lindi (Lindi Mjini) katika kipindi hiko cha zamani. Masharifu ni watu walioaminika kuwa na uwezo au nguvu za kufanya mambo ambayo yasiyo yakawaida katika jamii kwa Imani kuwa watu hawa walikuwa ni wateule wa Mungu ambao wamechaguliwa kuiongoz jamii hasa ya Waislamu. Masharifu huwaminika kuwa ni watu ambao wapo katika mtiririko wa vizazi vya manabii kwa upande wa Imani ya Uislamu. Masharifu wanakuwa na asili ya Waarabu ambao waliwahi kuishi katika Mji wa Lindi kipindi hiko cha Utawala wa Waarabu.



C. VIVUTIO VYA UTAMADUNI




S/N
KIVUTIO
MAELEZO
PICHA
1
Ngoma za 
asili
Ngoma ya tambiko ambayo hutumika na kabila la Wamwera  ikiwa ni wenyeji wa Mkoa wa Lindi ,Ngoma hii huchezwa wakati wa  maombi maalumu kwa mwenyezi Mungu mfano kama mvua hazinyeshi hivyo  jamii ya Wamwera hukusanyika pamoja na kufanya  nguo  ya kaniki nyeusi/nyeupe na nyekundu na usinga pamoja na ngoma jembe (NTONYA).

2
Mwani
Mwani ni mmea unaolimwa ndani ya bahari, mmea huu unatumika kama dawa, hutumika kutengenezea sabuni na pia ni zao la biashara ambapo linalimwa katika kata za Kitumbikwela na Mchinga ndani ya Manispaa ya Lindi.

Kilimo cha mwani
3
Vyakula vya asili
Wananchi wa Manispaa ya Lindi utamaduni wa kula vyakula vya asili ya pwani. Vyakula hivyo ni kama pweza, aina mbalimbali za samaki, mboga za asili kama kisamvu, ugali wa mhogo, ming'oko n.k.

Pweza

Ugali wa muhogo

Kisamvu


Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imebarikiwa kuwa na rasilimali za kihistoria ambazo kama zitalindwa, kutunzwa na kuendelezwa vizuri, zinaweza kuwa fursa nzuri ya kimaendeleo kwa Manispaa. Kupitia utalii, watu watapata ajira na thamani ya rasilimali hizi itaongezeka maradufu. Manispaa itajiongezea mapato na pia shughuli za ukarabati na utunzwaji wa malikale zitawezekana kupitia mapato yatakayotokana na utalii. Hivo viongozi, wadau wa serikali, mashirika binafsi pamoja na wananchi kwa ujumla wahamasishwe kutambua umuhimu wa malikale na majengo ya kihistoria na kuyatunza kwa dhati ili vizazi vijavyo viweze kufaidi matunda ya juhudi hizo.


Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa