• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

WAZIRI INNOCENT BASHUNGWA AKOSHWA NA PONGEZI ZA MKOA WA LINDI KWA MHE. RAIS SAMIA

Imetumwa: June 29th, 2022

Hafla ya kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan iliyoandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack imefanyika leo tarehe 29.06.2022 katika uwanja wa mpira wa miguu Ilulu uliopo ndani ya Manispaa ya Lindi.Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali na viongozi wa Kidini.Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. Innocent Bashungwa.

Hafla hiyo ilitanguliwa na maandamano mafupi ya kuingia uwanjani yaliyotanabaishwa na nyuso za furaha na bashasha na yaliyokuwa yamesheheni mabango yenye jumbe mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan.

Katika hotuba yake Mhe. Zainab Telack, alibainisha mambo muhimu ambayo yamefanywa na Serikali ya awamu ya sita chini ya Mhe. Samia Suluhu Hassan ndani ya mkoa wa Lindi katika kipindi kifupi cha miezi 15 tangu aingie madarakani. Miongoni mwa mambo yaliyobainishwa na Mhe. Zainab Telack ni pamoja na Mafanikio makubwa katika sekta ya Elimu, Afya, Maji, Umeme na Nishati, TASAF, Mawasiliano na uboreshaji wa maeneo mbalimbali ya kutolea huduma kwa wananchi wa mkoa wa Lindi.

  • Kwa upande wa Elimu: Serikali imetoa fedha ambayo imesaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi kwa kujenga vyumba vya madarasa 401 katika shule za sekondari ,msingi na katika vituo shikizi. Ujenzi huu wa madarasa umewezesha wanafunzi wote waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2021 kuingia madarasani kwa awamu moja. Pia mkoa wa Lindi umepewa fedha za kujenga shule mpya za sekondari 11 ikiwepo shule ya Sekondari Maalum ya Wasichana ambayo inajengwa katika eneo la Kilangala ndani ya Manispaa ya Lindi.Pia serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 6.2 kwa mkoa wa Lindi na kutumika kugharamia huduma mbalimbali za mpango wa elimu bila malipo.
  • Sekta ya Afya: Mkoa wa Lindi umepokea jumla ya shilingi bilioni 23.8 kwa ajili ya kuboresha miundombinu ikiwepo ujenzi wa Hospitali mpya ya Rufaa yenye thamani ya shilingi bilioni 7.6 eneo la Mitwero Manispaa ya Lindi.Ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Lindi ambapo serikali tayari imetoa shilingi milioni 500, ukamilishaji wa Hospitali tatu za Wilaya ambazo ni Liwale(Fedha iliyopokelewa na Shilingi Milioni 300) , Kiwalala(Fedha iliyopokelewa ni Shilingi Milioni 800) na Hospitali ya Wilaya ya Ruangwa(Fedha iliyopokelewa na Shilingi Milioni 800). Ujenzi wa vituo vipya vya Afya 11 vyenye thamani ya shilini bilioni 5.2, ujenzi wa nyumba za watumishi wa Afya 5 ambapo fedha kiasi cha shilingi milioni 450. Ujenzi wa ICU kwa Halmashauri ya Nachingwea(Shilingi milioni 200 imepokelewa), wodi za huduma za dharura(EMD)(Shilingi milioni 900 imepokelewa) , Ukamilishaji wa zahanati 26(Bilioni 1.2 imepokelewa).Aidha Serikali imetoa shilingi bilioni 4.1 kwa kipindi cha mwezi Machi 2021 hadi Mei 2025 kupitia MSD kwa ajili ya kununua dawa, vifaa tiba, vitendanishi na vifaa vya kutolea afya ya kinywa na meno.
  • Upande wa Sekta ya Maji: Serikali imetoa shilingi bilioni 20.3 kwa mkoa wa Lindi kwa ajili ya uboreshaji wa huduma ya maji katika makao makuu ya miji ya wilaya na maeneo ya vijijini. Manispaa ya Lindi na Wilaya ya Liwale na Kilwa zimepokea kiasi cha shilingi bilioni 6.3 kwa ajili aya utekelezaji wa miradi minne ya maji. Fedha hizi zimeongeza mtandao wa maji katika miji ya Mitwero, Mkwaya , Kitunda, Kiduni, Ngongo, Mayani na Mchinga katika Manispaa ya Lindi.Shilingi bilioni 14.2 zimetolewa kwa ajilia ya kuboresha huduma za maji vijijini ndani ya mkoa wa Lindi na kuwezesha kuongeza kiwango cha upatikanaji wa maji vijijini kutoka 67% na kufikia 82% ifikapo juni 2023.
  • Sekta ya Barabara: Upande wa TANROADS Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 18.1 na fedha hizi zinatumika kujenga barabara kwa kiwango cha lami,kutengeneza madaraja, kutengeneza barabara kwa kiwango cha changarawe.Kwa upande wa TARURA mkoa wa Lindi umepokea jumla ya shilingi bilioni 23.3 kwa ajili ya matengenezo ya barabara na ujenzi wa madaraja.
  • Ujenzi wa Majengo ya Utawala: Katika kuboresha sehemu za kutolea huduma kwa wananchi wa mkoa wa Lindi serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 4.002 kwa ajili ya ujenzi wa majengo ya utawala ya Halmashauri za Ruangwa(Shilingi milioni 822.1 imepokelewa), Liwale(shilingi bilioni 1 imepokelewa), Kilwa(bilioni 1 imepokelewa) na Halmshauri ya Mtama(Milioni 272 imepokelewa)
  • Katika upande wa TASAF: Serikali imetoa jumla ya shilingi bilioni 2.07 na kusaidia kwa kiasi kikubwa kwenye uboreshaji wa maisha ya kaya maskini katika mkoa wa Lindi kwa kuwapatia fedha za kuanzisha miradi midogo midogo ambayo inawapatia kipato na kuwakwamua kiuchumi.Katika hotuba yake Mhe. Zainab Telack amemtaarifu mgeni rasmi kuwa walengwa wa TASAF wamehudhuria hafla hiyo ili kumpongeza na kumshukuru Rais Samia.
  • Mawasiliano ya Simu: Katika kuendelea kuboresha mawasiliano ya Simu, Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) kwa mkoa wa Lindi limepokea kiasi cha shilingi bilioni 2.4 na kusaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza usikivu na upatikanaji wa mtandao katika maeneo mengi ya mkoa wa Lindi.Baadhi ya maeneo yaliyonufaika ni pamoja na Makutano(Liwale), Mwengei(Kilwa), Nandete(Kilwa), Muungano(Kilwa), Mputwa(Lindi) na Kimambi(Liwale).
  • Katika Sekta ya Michezo: Serikali imetoa jumla ya shilingi milioni 352 kwa ajili ya kuendeleza uwanja wa Kassim Majaliwa uliopo wilaya ya Ruangwa ambao upo kwenye hatua za mwisho.

Mhe. Zainab Telack aligusia pia mafanikio katika ukusanyaji wa mapato ya ndani kwa Halmashauri zote za mkoa wa Lindi kwa kipindi cha Machi 2021 hadi Mei 2022.Ambapo amesema Halmshauri zilikadiria kukusanya shilingi bilioni 21.9 ambapo hadi kufikia Mei mwaka huu tayari zimekusanya shilingi bilioni 15.9 ikiwa ni sawa na 72% ya kiasi kilichotarajiwa.Katika fedha hizo shilingi bilioni 1.5 zimepelekwa kwenye shughuli za maendeleo hasa kuviwezesha vikundi vya Vijana, Wanawake na Watu wenye ulemavu ambao nao pia walijumuika uwanjani na kumpongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Aidha Mhe. Zainab Telack amemshukuru sana Mhe. Samia kwa kusaini mkataba wa makubaliano ya awali na maelezo aliyoyatoa kuhusiana na mradi mkubwa wa gesi aslia (LNG) ambao utatekelezwa katika eneo la Likong’o Manispaa ya Lindi.Kwa kitendo hicho Mhe. Telack amesema Rais Samia amekosha nyoyo za wananchi wa mkoa wa Lindi.alisema “Sisi kama Wanalindi matarajio yetu ni makubwa na tunaendelea kujiandaa ikiwa ni pamoja na kuwaandaa wananchi wetu kuipokea fursa hiyo kubwa ambayo imeletwa na Mhe. Samia Suluhu Hassan na ni fursa ambayo Wanalindi hawataisahau”. Pia ujenzi wa bandari kubwa ya uvuvi Kilwa yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 255 ni jambo linalopelekea Wananchi wa Lindi Kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan.

Hakuishia hapo tu, Mhe. Zainab Telack alimueleza Mgeni rasmi jinsi Watumishi na Wananchi wa mkoa wa Lindi wanavyomshukuru Mhe. Samia kwa kuboresha maslahi ya Watumishi wa Umma.

Kwa upande wake Mgeni Rasmi Mhe. Innocent Bashungwa, Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI amefurahishwa sana na kitendo cha Mkuu wa mkoa kuandaa hafla hiyo na kuahidi kuzifikisha salamu za shukrani na pongezi moja kwa moja kwa Mhe. Rais Samia.Mhe. Bashungwa amempongeza mkuu wa mkoa wa Lindi kwa hotuba nzuri iliyosheheni mambo makubwa na muhimu kwa kuwahabarisha wananchi wa Mkoa wa Lindi na ametoa agizo wa Wakuu wa mikoa yote nchini kuiga ubunifu wa mkuu wa mkoa wa Lindi.Pia Mhe. Bashungwa ametoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya zote nchini kuandaa majukwaa ambayo yatatumika kuelezea kazi nzuri inayofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani.

Aidha Mhe. Bashungwa ameungana na viongozi wa dini kumuombea afya njema Rais Samia ili aweze kuendelea kuwaletea maendeleo Wananchi wa Tanzania.




Wananchi wa mkoa wa Lindi wakiwa kwenye maandamano kuingia uwanjani
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack akitoa hotuba mbele ya Mgeni Rasmi


Imeandaliwa na Kitengo cha Habari na Mawasiliano

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa