• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

SIKU YA MTOTO WA AFRIKA MANISPAA YA LINDI YAFANYIKA KATA YA MATIMBA.

Imetumwa: June 15th, 2023

Maadhimisho hayo yamefanyika Juni 15, 2023 katika shule ya sekondari Nangaru kata ya Matimba na yamesimamiwa na idara ya maendeleo ya jamii Manispaa ya Lindi, chini ya afisa maendeleo ya jamii Moses Mkoveke yakihusisha wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, wazazi na walezi kutoka katika kata ya Matimba, Manispaa ya Lindi.

Katika maadhimisho hayo elimu kuhusu masuala ya watoto pamoja na burudani mbalimbali kama vile ngonjera vilitolewa mbele ya mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa.

Mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo alikuwa ni diwani wa viti maalumu tarafa ya Nangaru Ashiza Mtagaluka. Kaulimbiu ya maadhimisho ya mtoto wa Afrika mwaka huu ni "ZINGATIA USALAMA WA MTOTO KATIKA ULIMWENGU WA KIDIJITALI".

Aidha, Mtagaluka amewaomba wananchi wote kuwa walinzi wa kweli kwa watoto wetu kwani wanahitaji muongozo wa maadili na usimamizi mzuri katika makuzi yao, hasa ikizingatiwa kuwa umri walio nao ndio wenye changamoto kubwa kwa matendo ya ukatili yanayojitokeza kama vile ubakaji , ulawiti, utumikishwaji katika ajira hatarishi , ukeketaji , ndoa na mimba za utotoni.

 Kwenye risala yao wanafunzi wa shule ya sekondari Nangaru wameomba matukio na Sherehe kama hizo ziendelee kufanyika katika kata yao ya Matimba ili kuongeza ari kwa wana matimba katika kutokomeza ukatili wa watoto.

Sambamba na hilo wanafunzi hao walimpongeza mgeni rasmi Mhe. Ashiza Mtagaluka kwa kutumia muda wake kushiriki maadhimisho hayo, lakini pia walitoa shukrani kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Juma Mnwele kuruhusu kata ya Matimba kuwa wageni wa maadhimisho hayo kwa mwaka 2023.

Katika hatua nyingine afisa maendeleo ya jamii Manispaa ya Lindi Moses Mkoveke aliongoza kikao cha siku ya kupinga ukatili wa wazee, ambapo alimuwakilisha mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga, kikao ambacho kilifanyika katika shule ya sekondari Nangaru huku wageni waalikwa wakiwa ni wazee kutoka kata ya Matimba na kilihusisha, kijadili mambo mbalimbali kuhusu haki za wazee katika Manispaa ya Lindi.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa