• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

RC ZAINAB TELACK AZINDUA KAMPENI YA ONGEA NA MKUU WA MKOA

Imetumwa: July 9th, 2021

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack azindua kampeni ya ongea na mkuu wa mkoa sambamba na kutambulisha namba ya simu ambayo itatumika kuwasilisha kero mbalimbali za wananchi na watumishi wa mkoa wa Lindi.Katika uzinduzi wa kampeni hiyo Mhe. Zainab Telack amewataka wananchi na watumishi wa umma kumpa ushirikiano ili kuleta maendeleo katika mkoa wa Lindi.Mhe. amewahakikishia watumishi na wananchi wa mkoa wa Lindi maisha ya furaha kwa kusema "Kwa watumishi wa umma na wananchi wa mkoa wa Lindi kwa ujumla ni zamu yenu sasa kuwa na furaha kwa sababu mkoa wenu sasa una Mama, na wajibu wa mama ni kulea, si mnajua mama anabeba mimba miezi tisa, hawezi kula, hawezi kulala na anazaa kwa uchungu, lakini anachapa mtoto, hizo ndizo sifa za mama".Mhe. Zainab Telack aliendelea kusema "Lakini niwaombe watumishi wa umma kwa kuanzia, fanyeni kazi za umma kwa mujibu wa taratibu, lakini fanyeni pia kazi za kuwaongezea kipato, sitaki kuona watumishi wanaolialia, ardhi Lindi ipo, itumieni kwa kulima Alizeti,ufuta, mihogo na korosho, mimi natamani kuona watumishi waliopo Lindi wanabaki kuwa wanalindi".Mhe. Zainab Telack amewaomba watumishi wote waliopo Lindi kuondoa dhana ya kwamba Lindi ni mkoa wa adhabu, ameahidi kuifanya Lindi ionekane kwamba ni mkoa wa kufanyia kazi na sio mkoa wa adhabu kwa kuhakikisha anatengeneza mazingira mazuri ya kufanyia kazi yatakayoondoa manung'uniko.

Katika uzinduzi wa kampeni ya ongea na mkuu wa mkoa Mhe. Zainab Telack alisema kwamba kampeni hiyo ni mwendelezo wa jitihada za serikali katika kujenga mahusiano mazuri yanayozingatia haki na usawa, kusogeza karibu na kuboresha huduma kwa wananchi wa mkoa wa Lindi."Kuanzishwa kwa kampeni hii kutawawezesha wananchi kupata maendeleo kwa sababu wataachana na mgogoro, wataenda kufanya kazi", aliindelea kusema Mhe. Zainab Telack.Pia mkuu wa mkoa aliwaomba watumishi kuwa wazalendo kwa kujali utu, heshima na masilahi ya kila mtumishi na mwananchi. "Mwananchi akija kwako msikilize, mhudumie, mpe heshima yake kwani ana haki ya kuja kwako kulalamika, na hakuna taasisi yoyote ambayo wananchi hawaendi kulalamika, ukienda kwenye maji, wapo wanaolalamika, ukienda kwenye umeme, wapo wanaolalamika, ukienda kwenye barabara, wapo wanaolalamika, mtu kuja kukuambia kwamba barabara yetu haipitiki, sio kosa, kuja kukuambia kwetu umeme unakatika katika, sio kosa, mruhusu ajieleze ili uweze kuona namna ya kumsaidia" alisema Zainab Telack.

Aidha, Mhe. Zainab Telack amesisitiza kwamba kero za watumishi wa umma zinapaswa kusikilizwa na kutatuliwa.Katika kuleta ufanisi wa kushughulikia kero za watumishi na wananchi wa mkoa wa Lindi Mhe Zainab Telack ametoa maagizo kwamba Mtumishi wa umma hapaswi kupanga foleni katika kupata huduma katika taasisi yoyote ili nayeye aweze kuwahi kuwahudumia wananchi waliopanga foleni katika ofisi yake.Mhe. Zainab aliendelea kusisitiza kuwa kila mtu atekeleze wajibu wake ili apate haki anazostahili."Ndugu zangu, natamani kuona haki na misingi ya utawala bora inazingatiwa ili tuwaache wananchi wetu huru, waweze kutekeleza majukumu yao ya uzalishaji mali wakiwa na furaha" alisema Mhe. Zainab Telack.

Pia Mhe. Zainab Telack amezindua kaulimbiu ya "Uchumi imara kwaajili ya maendeleo yetu, tufanye kazi kwa bidii", ambapo amesisitiza kwamba wananchi wa mkoa wa Lindi wanahitaji kuwa na uchumi imara kwa maendeleo yao na ili wafikie uchumi huo, wanahitaji kufanya kazi kwa bidii. Kwa hiyo ni lazima wananchi wapewe nafasi ya kuondoa changamoto zote zitakazowakabili ili waweze kufanya kazi kwa bidii na kufikia uchumi imara.Katika hili Mhe. Zainab Telack ametoa mfano wa mwananchi anayeshinda mahakamani kwamba ataishi kwa wasiwasi kwamba anaweza kufungwa na hivyo kushindwa kufanya kazi kwa bidii, lakini changamoto zake zikitatuliwa ataondokana na wasiwasi na kumpekea kufanya kazi kwa bidii.Mhe. Zainab Telack ameendelea kusisitiza kwamba hategemei kupokea malalamiko ambayo yameshafanyiwa kazi na ufumbuzi wake ukapatikana na kusema kwamba kampeni hiyo isiwe chanzo cha kufukua makaburi kwa kisingizio cha mkuu wa mkoa au mkuu wa wilaya mgeni.Pia wananchi waliaaswa kwamba yapo mambo ambayo sio lazima kuyapeleka mahakamani, ambapo wanaweza kutumia ofisi zao na suluhu ikapatikana.Kampeni ya ongea na mkuu wa mkoa haiondoi fursa ya watendaji wa ngazi ya chini kuwasikiliza wananchi. Wananchi waendelee kusikilizwa kwenye kijiji, kwenye kata na kwingineko kote ambako wanasikilizwa, alisisitiza Mhe. Zainab Telack.


Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack akitaja namba ya simu ambayo ni (0736 281 281) itakayotumika kusikiliza kero mbalimbali za watumishi na wananchi wa mkoa wa Lindi.


Mbunge wa jimbo la Lindi mjini Mhe. Hamida Abdallah akitoa salamu kwa niaba ya wabunge wote wa mkoa wa Lindi.


Meya wa Manispaa ya Lindi Mhe. Frank Magali akitamatisha uzinduzi wa kampeni ya ongea na mkuu wa mkoa.


Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa