Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Ndugu Juma Mnwele ameahidi kusimamia vyema miundombinu ya miradi iliyotekelezwa na shirika la Heart to Heart,Ameyasema hayo leo alipokuwa kwenye hafla ya kukabidhiwa mradi wa maji na vyoo shule ya msingi Mvuleni na mradi wa maji zahanati ya Mvuleni.
Mnwele ametoa shukrani za dhati kwa shirika la Heart to Heart kwa mambo makubwa waliyofanya tangu walipoanza mpaka kufikia kumaliza mkataba wao.Pia amewaomba kuendelea kutekeleza miradi mingine zaidi kwani bado kuna uhitaji mkubwa wa miundombinu hiyo.
Aidha Katibu Tawala wa Wilaya ndugu Thomas Safari ambaye alikuwa mgeni rasmi akikaimu nafasi ya Mkuu wa Wilaya amewaomba walimu na wazazi kuhakikisha wanawafundisha vyema wanafunzi kutunza miundombinu hiyo lakini pia matumizi sahihi ili iweze kudumu kwa muda mrefu.
DAS akitoa neno la shukurani kwa shirika la Heart to Heart.
Shirika la Heart to Heart limeanza kufanya kazi ya kutekeleza miradi ya maji,vyoo na misaada mbalimbali kwa vituo vya afya na shule za msingi mwaka 2019 ambapo mpaka kufikia mwaka 2021 wameshatekeleza ujenzi wa vyoo 12 kwa shule za msingi 6,miradi ya maji kwa zahanati 3 na miradi ya maji kwa shule za msingi 14 lakini pia wametoa elimu juu ya usafi wa mazingira kwa walimu wakuu na elimu juu ya kuepuka magonjwa yatokanayo na maji kwa wafawidhi lengo likiwa kuwafikia watu wengi zaidi ili kuweza kupata elimu husika kupambana na magonjwa mbalimbali yatokanayo na maji ikiwemo kichocho na kuhara.
Wamehitimisha rasmi mkataba wao wa miaka 3 (WASH) tarehe 25/11/2021 katika ukumbi wa sea view ambapo viongozi wa ngazi mbalimbali na wataalamu walipata wasaa wa kushiriki lakini pia kufanya makabidhiano ya miradi kwa maandishi.
Mgeni rasmi akikata utepe kuzindua vyoo shule ya msingi Mvuleni.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255717469888
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa