• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

“MIAKA 61 YA UHURU LINDI IMEPIGA HATUA KUBWA KIMAENDELEO”-DC NDEMANGA

Imetumwa: December 9th, 2022

Maadhimisho ya miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika mwaka huu ambayo ki wilaya yamefanyika kwenye Halmashauri ya manispaa ya Lindi ambayo yalifanyika kwenye viwanja vya shule ya msingi Mpilipili ambapo pia yalienda sambamba na siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia, yalikua ni moja ya maadhimisho ambayo yalifana sana kulingana na uwepo wa burudani mbalimbali  ambazo zilipelekea wageni waalikwa kufurahia na kupata elimu.Pia kupitia maadhimisho hayo. Mkuu wa wilaya ya Lindi, Mhe. Shaibu Ndemanga alitumia nafasi hiyo kuongea na wananchi kuhusiana na  hali ya maendeleo ambayo wilaya ya Lindi yamepata baada ya uhuru  ukilinganisha na kipindi ambacho tulikuwa hatuja pata uhuru. Ndemanga aligusia maendeleo katika sekta mbalimbali ikiwemo Elimu,Afya ,Miundombinu pamoja na uwepo wa Halmashauri mpya ambapo mwanzoni tulikuwa na Halmashauri moja tu ambayo ni Halmashauri ya Lindi lakini kwa sasa hivi tumepiga hatua na tumepata Halmashauri ya Mtama. .

Miongoni mwa mambo aliyo zungumzia kwenye upande wa elimu ni kwamba wilaya ya Lindi sasa imefanikiwa kuwa na shule za msingi na sekondari takribani kila kata pia kwa upande wa vyuo  tumefanikiwa kupata vyuo vya ufundi stadi (VETA) na pia wilaya imebahatika kuwa na chuo kikuu huria.

Ndemanga pia aligusia upande wa Afya ambapo alizungumzia jitihada mbalimbali ambazo zina  fanyika na madaktari pamoja na manesi wetu kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora, lakini pia uwepo wa madkati na manesi wa kutosha katika maeneo ya kutolea huduma za afya.

Vile vile alizungumzia uwepo wa vifaa tiba vya kutosha katika zahanati na vituo vyetu vya kutolea huduma za afya.

Sambamba na hilo alizungumzia maendeleo tuliyo yapata kwenye upande wa miundombinu, ambapo kwa sasa barabara  ni nzuri na pia zina pitika ukilinganisha na kipindi cha nyuma ambapo, ilikua ina mlazimu abiria kusafiri  ya siku sita kutoka Lindi kwenda Dar es salaam.

Kwa upande mwingine Mkurugenzi wa  manispaa ya Lindi Mhe, Juma Mnwele, alizungumzia  suala la ukatili kwa watoto na wamama, ambapo alisema “ italeta faraja tuki adhimisha ,miaka 61 ya Uhuru wa Tanganyika tukiwa  na jamii ambayo ina fahamu, inatambua na imepunguza suala hili la unyanyasaji  wa kijinsia ” Lakini pia alitumia nafasi hiyo kutoa pongezi kwa Halmashauri ya Mtama kwa kujitokeza kwa wingi kwenye maadhimisho hayo ya miaka 61 ya  Uhuru wa Tanganyika.

Vilevile, mgeni rasmi alipata nafasi ya kutoa zawadi  ya daftari kwa wanafunzi mbalimbali ambao walishiriki katika zoezi la kuandaa ushairi wa kupinga ukatili  kutoka  kwenye shule za msingi na sekondari ambapo kwenye shule za msingi  zilizo shiriki zilikuwa ni shule 11 na kwa upande wa sekondari zilikuwa shule 3.

Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga akikabidhi zawadi ya madaftari kwa wanafunzi walioshinda zoezi la uandishi wa mashairi

Mwishoni, mgeni rasmi alipata zawadi ya kitabu cha ushairi (Diwani) ya  Amri Abeid Kaluta, ambapo zoezi hilo lilifanywa mkurugenzi wa Tanzania  Child Welfare (TCW) ambae pia ni  Mwenyekiti wa (UKUTA) taifa.

Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga akikabidhiwa zawadi ya vitabu vya ushairi

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa