• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MAOMBOLEZO YA HAYATI DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KIMKOA LINDI

Imetumwa: March 25th, 2021

Uongozi wa mkoa wa Lindi umefanya maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli katika uwanja wa Ilulu uliopo katika Manispaa ya Lindi.Maombolezo hayo yamehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa dini, siasa, watumishi wa serikali pamoja na wananchi wa Mkoa wa Lindi. Shughuli hiyo ilitanguliwa na salamu za rambirambi kutoka kwa mwakilishi wa Mkuu wa mkoa wa Lindi, viongozi wa madhehebu mbalimbali ya kidini na kufuatiwa na ibada fupi iliyoongozwa na Mhashamu Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi Bruno Pius Ngonyani. Akizungumza katika maombolezo hayo, Mwakilishi wa Mkuu wa Mkoa wa Lindi ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga, alisema kuwa wananchi wa Mkoa wa Lindi na Tanzania kwa ujumla wamepata pigo kubwa kwa kuondokewa na mpendwa wao na kusisitiza kuyaenzi yote mazuri yaliyofanywa na Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.Aliendelea kusema kwamba Serikali iliyoongozwa na Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli imetekeleza miradi mingi katika mkoa wa Lindi ikiwemo ujenzi wa Hospitali za wilaya, Zahanati, shule, miradi ya maji, ujenzi wa miundombinu mbalimbali pamoja na barabara.

Aidha, Mhe. Shaibu Ndemanga aliendelea kusisitiza kwamba ipo miradi inayoendelea kutekelezwa na mingine ikiwa katika mipango ya kutekelezwa katika mkoa wa Lindi kama mradi wa gesi asilia (LNG) pamoja na ujenzi wa shule maalumu ya wasichana ambayo Hayati Dkt. Magufuli aliutaka uongozi wa mkoa wa Lindi kutenga eneo kwa ajili ya ujenzi huo na Mhe. Ndemanga aliuthibitishia uma kwamba eneo ambalo lipo Kilangala limeshatengwa na serikali imeahidi kujenga shule hiyo kwa gharama ya takribani Tzs Bilioni 4 na tayari uongozi wa mkoa umepokea Tzs Bilioni moja kwa ajili ya kuanza shughuli hiyo.Pia ameeleza kwa masikitiko makubwa kwamba alitamani jiwe la msingi la shule hiyo lingewekwa na Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kama angelikuwa bado yupo hai.Mhe. Shaibu Ndemanga amethibitisha kupokea ujumbe kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan wa kumtoa hofu na kumtia matumaini kwamba miradi yote iliyopangwa kutekelezwa mkoani Lindi itatekelezwa kikamilifu.

Aidha, Viongozi wa dini walisisitiza kwamba Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alikuwa mtetezi wa wanyonge na alikuwa mcha Mungu kwani muda mwingi alimkumbuka Mwenyezi Mungu na kuwataka watanzania wote kumtanguliza Mungu katika kila jambo. Viongozi hao walitoa pole kwa Rais mteule wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Mjane Mama Janeth Magufuli ambaye alikuwa mke wa Hayati na kwa watanzania wote kwa kuondokewa na mpendwa wao. Pia Mkuu wa wilaya ya Kilwa katika kutoa salamu za rambirambi na neno la shukrani alisema  kila Mtanzania anapaswa kujipima na kujiuliza kuwa ameifanyia nn Tanzania huku akiendelea kuyaenzi mambo yote yaliyofanya na Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwani kifo katika maisha ya binadamu sio nukta (kikomo) bali ni mkato.

Viongozi wa dini wakipunga mkono wa kwaheri ya kuonana kwa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Viongozi wa mkoa wa Lindi wakipunga mkono wa kwaheri ya kuonana kwa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Wanakwaya wakiimba wimbo wa maombolezo



Wanafunzi wa  Lindi sekondari wakipunga mkono wa kwaheri ya kuonana kwa Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli.


Wanafunzi wakiwa kwenye majonzi mazito kwa kumpoteza Rais muasisi wa Sera ya elimu bure.



Wananchi wa Lindi wakibubujikwa na machozi kwa kumpoteza mpendwa wao aliyekuwa Rais wa wanyonge.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa