Kamati ya siasa Mkoa wa Lindi wametembelea miradi ya maendeleo ikiwemo iliyotekelezwa kwa fedha za UVIKO-19 leo tarehe 10/01/2022.Miradi iliyotembelewa ni Pamoja na stendi ya maegesho ya malori Mnazimmoja,Shule ya sekondari Mingoyo,Kituo cha Afya Mvuleni,Mradi wa gesi(LNG) na mahakama ya Wilaya.
Awali,Kamati ya Siasa imetoa shukrani kwa wananchi kwa namna ambavyo wamejitoa kuhakikisha miradi hiyo inakamilika kwa wakati lakini pia kupunguza gharama za ujenzi na wamewashukuru viongozi kwa jinsi wanavyosimamia miradi hiyo kuweza kukamilika kwa wakati lakini pia kwa ubora wa majengo hayo.
Mwenyekiti wa kamati ya siasa Mkoa ametaka kuwe na mshikamano baina ya viongozi na wananchi katika kutekeleza miradi ya maendeleo.
Wanakamati wametoa rai kwa wananchi kutoacha kushiriki kwenye miradi ya maendeleo lakini pia viongozi kuendelea kuwa vipaumbele kwenye kushiriki na kuhakikisha miradi hiyo inamalizika ndani ya muda uliopangwa.
Aidha Mkurugenzi wa Manispaa Ndugu Juma Mnwele amesema ujenzi wa stendi ya maegesho ya malori Mnazimmoja ni utekelezaji wa agizo la Mhe.Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipotembelea Manispaa ya Lindi 05/10/2021, ameahidi stendi hiyo kukamilika mwishoni mwa mwezi wa pili.
Kamati imetoa pongezi kwenye ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa shule ya sekondari Mingoyo na ujenzi wa Kituo cha Afya Mvuleni kuwa majengo yamejengwa kwa ubora wa hali ya juu unaoendana na kiasi cha fedha kilichotolewa kutekeleza miradi hiyo.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255717469888
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa