• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MAKALA TASAF (PART 3): TASAF IMEYAWEZESHA MAISHA YANGU KUWA MEPESI ZAIDI

Imetumwa: June 11th, 2018

Bi Maimuna Mohamed Mpukwe ni mama mwenye umri wa miaka 54. Mama huyu anaishi na wajukuu zake watatu ambao wote wanasoma shule. Mjukuu mmoja anasoma kidato cha tatu katika shule ya sekondari Lindi, mjukuu mwingine anasoma darasa la nne katika shule ya msingi Mpilipili na wa tatu anasoma chekechea katika shule ya msingi Mpilipili. Bi Maimuna ambaye anaishi katika kata ya Makonde Mtaa wa Sheikhbad amekuwa akinufaika na Mpango wa TASAF III wa Kunusuru Kaya Maskini sana toka mwaka 2013 na hadi anahojiwa na mwandishi wa habari hizi alikuwa amepokea ruzuku mara 31.

Wakati wa mahojiano, Bi Maimuna alisema kuwa hali yake ya maisha kabla ya kutambuliwa na TASAF kama kaya maskini ilikuwa ngumu hasa katika upatikanaji wa huduma za afya, chakula na elimu kwa wajukuu zake. Alieleza kuwa wakati huo walikuwa wanapata mlo mmoja na mara chache milo miwili kwa siku. Aliendelea kusema kuwa, ilikuwa vigumu sana kwake kuweza kugharamia mahitaji ya shule pamoja na afya. Alisema kuwa wakati huo hakuwa na shughuli yoyote ya kiuchumi ya kuingiza kipato kutokana na kukosa mtaji wa kuanzisha biashara.

Kuhusiana na mtiririko wa Fedha za ruzuku katika kaya ya Bi Maimuna Mohamed Mpukwe, alikiri kuwa ruzuku yake imekuwa ikishuka kutoka Tsh 34,000.00 ambapo kwa sasa anapokea Tsh 28,000.00. Alisema kuwa japo pesa hizi zimekuwa zikipungua, lakini zinamsaidia sana kugharamia mahitaji ya wajukuu zake wanaoenda shule, kununulia chakula, kugharamia chakula cha kuku anaowafuga nyumbani kwake na kulipia gharama za matibabu kupitia Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF). “Kabla sijaingia katika mpango huu wa TASAF nilikuwa sina uwezo wa kugharamia mahitaji yote ambayo ninaweza kuyagharamia leo hii”, alisema Bi Maimuna Mohamed Mpukwe wakati akihojiana na mwandishi wa habari hizi.

Bi Maimuna Mohamed Mpukwe alisema kuwa TASAF imemuwezesha kuanzisha huduma ya mamalishe katika makazi yake ambapo anapika na kuuza vyakula vya aina mbalimbali. Ameanzisha pia ufugaji wa kuku wa kienyeji ambao humwingizia pesa kwa kuuza mayai pamoja na kuku hai. “Kusema kweli hii biashara ya chakula inaniwezesha kupata faida ya hadi shilingi elfu ishirini kwa mwezi ambazo zinaniwezesha kugharamia mahitaji mbalimbali yangu binafsi pamoja na wajukuu wangu ninaoishi nao; kusema ukweli maisha kwangu yamekuwa mepesi sana”, alisema Maimuna Mohamed. Alisema kuwa pesa anazopata zinamwezesha kujikimu kwa kipindi chote ambacho hakuna Malipo.

Aidha, Bi Maimuna alisema kuwa anayo mambo mengi ya kujivunia ikiwa ni pamoja na kumudu kuanzisha biashara ya mamalishe pamoja na ufugaji wa kuku wa kienyeji.

Bi Maimuna akiwa katika shughuli zake za mama lishe

Kuhusu ushauri kwa Walengwa wengine waliomo kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini sana, Bi Maimuna Mohamed alisema kuwa anawashauri wajitahidi kuanzisha biashara ndogondogo ambazo hazihitaji mitaji mikubwa kama vile biashara ya mamalishe na babalishe. Aidha aliitaka Serikali iendelee kuzitambua kaya zingine maskini ambazo bado hazijaingia katika mpango wa Kunusuru kaya maskini ili nazo ziweze kunufaika na programu hii.

Hata hivyo Bi Maimuna Mohamed Mpukwe alisema kuwa ana mipango kadha wa kadha ya kuboresha maisha yake ikiwa ni pamoja na kupanua biashara yake ya mamalishe na kuongeza idadi ya kuku ili kuongeza uzalishaji  wa mayai


Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa