• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MAKALA TASAF (PART 2): TASAF IMEKUWA MKONO WANGU WA PILI KATIKA KUPAMBANA NA UMASKINI

Imetumwa: June 4th, 2018

Bi Zalia Zuberi Likoja alizaliwa miaka arobaini (40) iliyopita na kujaliwa kupata watoto nane (8) ambao alizaa na bwana ambaye amemtelekeza yeye na watoto. Kwa sasa Bi Zalia anaishi katika nyumba aliyopewa na baba yake mzazi iliyopo katika Kata ya Mtanda, Mtaa wa Mtanda Juu. Bi Zalia ni miongoni mwa Walengwa 67 wa Mtaa wa Mtanda Juu wanaonufaika na Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini sana chini ya programu ya TASAF III. Mama huyu amesajiliwa kwa namba PSSN-LMC-02422-1 na amekuwa akinufaika na mpango huu wa Kunusuru kaya maskini sana toka mwaka 2013 ambapo ameshapokea ruzuku kwa awamu 31.

Bi Zalia Zuberi Lijoka anaishi na watoto sita (6) ambapo watoto watano (5) wapo shule ya msingi Mtanda na mtoto mmoja mwenye umri wa miezi 17 bado anahudhuria kliniki.  Kaya ya bi Zalia ina wategemezi wengine wanne (4) ambao ambao wanamtegemea kwa chakula na huduma zingine za msingi kama vile malazi na matibabu wanapougua.

Bi Zalia alikaririwa akisema kuwa, “kabla sijajiunga na Mpango wa TASAF wa Kunusuru Kaya Maskini sana, maisha yalikuwa magumu sana; nilikuwa ninamudu kununua kilo moja ya unga kwa ajili ya kupikia uji asubuhi na Ugali jioni na wakati mwingine tulikuwa tunapata mlo mmoja tu”.

Aliendelea kusema kuwa chanzo kikubwa cha mapato katika kaya yake kilikuwa ni vibarua vya kulima na kufua nguo majumbani mwa watu. Alikiri kuwa kipato kilikuwa kidogo sana kumwezesha kugharamia mahitaji ya watoto shuleni, kulipia huduma za afya na hata kuboresha makazi anayoishi. Mama huyu alisema kuwa, toka ajiunge na TASAF amekuwa na uhakika wa kupata milo mitatu kwa siku, amemudu kuwanunulia watoto wake chakula chakutosha pamoja na kulipia gharama za shule kwa watoto wake wote watano waliopo shule ya msingi.                                                                                                  

Ilifahamika kuwa, kaya hii imepokea ruzuku kwa Awamu 31 na ilianza kupokea ruzuku ya Tsh 34,000.00 ambayo baadaye ilipanda hadi Tsh 48,000.00 na kwasasa inapokea Tsh 52,000.00. Ruzuku hii imeifanya kaya hii kushuhudia mabadiliko ya aina tofauti tofauti kama alivyoelezea Bi Zalia Zuberi Lijoka; “ruzuku ya TASAF imeniwezesha kusomesha watoto wangu shule ya msingi, ninamudu kuwanunulia mavazi na sare za shule, kugharamia huduma za matibabu pamoja na kuboresha malazi yao kwa kuhakikisha kuwa wanalala ndani ya vyandarua”.

Aidha, Bi Zalia alisema kuwa  pesa anazozipata kutokana na TASAF III na elimu ya Kilimo cha mjini aliyoipata wakati wa kutekeleza miradi ya ajira ya muda vimemwezesha kuanzisha bustani yake ya mbogamboga ambayo inamwingizia wastani wa Tsh 3,000.00 kwa wiki. Chanzo kingine cha Fedha kwa Bi. Zalia ni pamoja na kuvunja mawe na kuuza kokoto ambapo ndoo ndogo ya lita 10 huuzwa Tsh 700.00. Alisema kuwa kipato anachopata huwa kinamwezesha kujikimu mwezi ambao hakuna hakuna Malipo.

Bi Zalia Zuberi Lijoka akichuma mboga kwa ajili ya kumuuzia mteja wake

“Kutokana na mimi kuwa kwenye mpango pamoja na kuongezeka kwa ruzuku, nimemudu kuanzisha bustani ya kilimo cha mboga mboga, biashara ya kuvunja na kuuza kokjoto pamoja na kujiunga katika Kikundi cha Kuweka Akiba na Kuwekeza”, alisema Zalia Zuberi Lijoka. 

  • Hata hivyo Bi Zalia aliielezea mipango yake ya baadae ya kuondokana na umaskini kuwa ni pamoja na;
  • Kuanzisha biashara ya mkaa
  • Kupanua eneo la bustani
  • Kuendelea kuwa katika vikundi vya COMSIP

Taarifa hii imeandaliwa na Ofisi ya TASAF Manispaa ya Lindi

Mei, 2018

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa