• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

Imetumwa: March 9th, 2019

Wanawake wametakiwa kujitokeza kutoa taarifa za matendo ya unyanyasaji na ukatili dhidi ya wanawake. Maneno hayo yamesemwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga katika maadhimisho ya siku ya wanawake duniani yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mitwero.

Akizungumza wakati anahutubia Mhe. Ndemanaga alisema kuwa takwimu za shirika la Afya duniani zinaonyesha kuwa asilimia 35 ya wanawake ulimwenguni ni wahanga wa vipigo na ukatili wa kingono. Kwa hapa nchini ukatili huu bado ni mkubwa jambo ambalo linaligharimu taifa kwa kiwango kikubwa katika nyanja tofautitofauti kwa kuwa unazorotesha Afya za wanawake. Kwa mwaka 2019 jeshi la polisi nchini limepokea matukio 4,423 ya ubakaji, 1,801 ya shambulio, 1,021 ya mashambulio ya kudhuru mwili na matukio ya kujeruhi 819.

Kwa upande wa Manispaa ya Lindi matukio ya ukatili kwa wanawake yaliyoripotiwa polisi kwa kipindi cha mwaka mmoja ni 21 tu. Lakini hii haimaanishi kuwa matukio hayo ni machache bali matukio mengi yamekuwa hayaripotiwi katika vyombo husika. Hivyo, Mkuu wa Wilaya akatoa wito kwa jamii kuripoti matukio haya na yasiishie majumbani tu kwa kuwa madhara yake ni makubwa sana.

Aidha, Afisa maendeleo ya jamii Bi. Miriam alisema wanawake ni nguzo muhimu katika maendeleo ya jamiii na taifa kwa ujumla lakini ni kwa muda mrefu wamekuwa wakiachwa nyuma kwa fikra kuwa hawana uwezo wa kuchangia katika maendeleo, jambo ambalo si kweli.

Maadhimisho ya siku ya wanawake duniani hufanyika kila tarehe 8 ya mwezi wa tatu ikiwa ni kumbukizi ya juhudi za wanawake kudai usawa katika jamii. Maadhimisho ya mwaka huu ni ya 108 kufanyika tangu siku hiyo ianze kusherehekewa rasmi mwaka 1911.

Kwa Wilaya ya Lindi siku hii hufanyika kwa kupokezana na Halmashauri ya Wilaya ya Lindi, ambapo mwaka huu yameratibiwa na Manispaa ya Lindi na kufanyika katika viwanja vya shule ya Msingi Mitwero. Maandalizi ya sherehe hii yalianza tangu tarehe nne ambapo wanawake wa Manispaa walianza kwa kushiriki katika ujenzi wa Zahanati ya Banduka, zoezi ambalo lilifanyika kwa siku mbili. Tarehe 6 kulikuwa na kongamano la kuwajengea uwezo wanawake ili waweze kujiajiri na hatimae kujiletea maendeleo endelevu. Tarehe saba walitembelea Watoto katika shule za sekondari za bweni na kuwapa elimu ya hedhi salama pamoja na namna ya kujikinga na mambo hatarishi. Na tarehe nane ambayo ndio siku ya kilele, kabla ya kufika katika viwanja vya sherehe wanawake hao walitembelea wagonjwa katika hospitali ya rufaa ya Sokoine na kuwapa misaada mbali mbali jambo ambalo lilipongezwa sana na Mkuu wa Wilaya.

“kitendo hiki kinaonyesha wazi ni kwa namna gani kina mama mnahuruma, mnaupendo wa kweli na mnatambua shida za kina mama wengine. Hongereni sana” alisema Mhe. Ndemenga.

Siku ya wanawake duniani mwaka huu ilikuwa na kauli mbiu “badili fikra kufikia usawa kijinsia kwa maendeleo endelevu”.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa