• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

KERO YA UMEME LINDI IMEFIKIA TAMATI

Imetumwa: May 22nd, 2018

Kwa kipindi kirefu wakaazi wa Mkoa wa Lindi wamekuwa wakikumbwa na adha ya umeme. Haikua ni ajabu kwa umeme kukatika zaidi ya mara 10 kwa siku. Jambo ambalo lilikuwa linawakera wananchi na kukwamisha shughuli nyingi za kiuchumi. Lakini kero hiyo sasa imefikia mwisho.

Hiyo ni baada ya Mkoa wa Lindi pamoja na Mtwara kuunganishwa rasmi katika grid ya taifa. Sherehe za kuunganishwa mikoa hii miwili katika grid ya taifa ilifanyika hapo jana katika Kijiji cha Mahumbika na kuongozwa na Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kasim Majaliwa akisindikizwa na Waziri wa Nishati Dkt Medard Kalemani pamoja na viongozi wengine wa kitaifa na Mkoa.

Mhe. Majaliwa akizungumza katika shughuli hiyo alisema kuwa kile kilio cha wananchi sasa kimefikia mwisho. Wananchi wategemee kupata umeme wa uhakika kwa masaa 24.

“Hapa ni umeme masaa ishirini na nne, kwa hiyo tafsiri ya Serikali ya kusema umeme ni wa kutosha hilo sasa tuna uhakika nalo, umeme rahisi, bei mmeisikia (ambayo ni shilingi 27,000/= tu),  wa uhakika kwa sababu unawaka masaa yote ishirina na nne. Kwa hili lazima tumpongeza Mh. Rais John Pombe Magufuli, Waziri wa Nishati na bodi nzima” alisema waziri mkuu baada ya kufanya uzinduzi wa uunganishwaji huo.

Aidha  wakizungumza kwa nyakati tofauti viongozi wa Mkoa wa Lindi wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe. Godfrey Zambi waliishukuru Serikali kupitia Wizara ya Nishati na Tanesco kwa kufanikisha zoezi hilo. “Tulipoambiwa kuwa kituo hiki (cha Mahumbika kinachoonganishwa katika grid ya taifa) kinajengwa tuliona kuwa haiwezekani, lakini Serikali kwa kupitia Wizara ya Nishati chini ya Waziri Kalemani, pamoja na shirika la umeme Tanesco, walituambia kwamba hili jambo linawezekana. Na sasa limewezekana” , alisema Mhe. Zambi.

Pia Mhe. Zambi alichukua fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji mbalimbali hususani wa viwanda ambao walikua wakisita kuja kuwekeza mkoani Lindi kwa kuhofia tatizo la umeme.

Licha ya kuwapongeza waliofanikisha mradi huo na kuwahakikishia wananchi na wawekezaji juu ya uhakika wa umeme mkoani Lindi kwa sasa, Waziri Mkuu aliwataka wananchi wawe mstari wa mbele katika kulinda miondombinu hiyo ya umeme na kuhakikisha kuwa aiharibiwi na kufanyiwa hujuma.

Pia aliwaka wananchi watumie nafasi hii ya umeme katika kuhakikisha wanafanya shughuli za kimaendeleo zenye kuleta tija na kuongeza kipato. Na akasisitiza kwa viongozi wahakikishe kuwa taasisi zote za kiserikali husani shule na vituo vya kutolea huduma za afya vinapata umeme.

Uunganishwaji huu umekuja muda muafaka hasa kwa Manispaa ya Lindi amabapo inaelekea katika utekelezaji wa sera ya uchumi wa viwada.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa