• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

GIRL GUIDE NA GIRL SKAUTI MKOA WA LINDI KUPANDA MITI YA MATUNDA NA VIVULI SHULE YA SEKONDARI ANGAZA.

Imetumwa: February 25th, 2023

Umoja wa skauti wanawake  mkoa wa Lindi (GIRL GUIDE) umepanda miti ya matunda na vivuli katika shule ya sekondari Angaza,tukio hilo limefanyika siku ya tarehe 25 ambayo ilikuwa ni siku ya kufikiri duniani9(WORLD THINKING DAY)Maadhimisho ambayo kaulimbiu yake ilikuwa ni "DUNIA YETU,MUSTAKABALI WETU WA AMANI,MAZINGIRA NA USAWA WA KIJINSIA".Zoezi hilo la upandaji wa miti hiyo limefanyika katika shule ya sekondari Angaza na kuhudhuliwa na viongozi mbalimbali akiwemo Afisa Maendeleo ya jamii Ndg, Moses Mkoveke ambaye alikuwa ana muwakilisha Mhe, Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe, Shaibu Ndemanga.Lakini pia tukio hilo limehudhuriwa na afisa mazingira Manispaa ya Lindi,mtendaji kata wa kata ya wailesi mwalimu mkuu wa shule ya sekondari  Angaza pamoja na wanafunzi wa shule ya sekondari  Angaza,Shule ya msingi Msinjahili, Stadium pamoja na shule ya msingi Mtuleni.Hiyo yote ni kuwakumbuka waasisi wao wa skauti ambao ni (Lord Baden Powell) pamoja na na girl guide na girl skauti (Olave Baden Powell)

Katika maelezo yao kwenye risala  wasichana wa Girl guides walisema, katika juma hilo la kutafakari wamefanya shughuli mbalimbali ambazo zimewawezesha kutambua umuhimu wa maelewano ya asili na haja ya mfumo ya ikolojia yenye usawa.

Kwenye eneo la shule ya sekondari Angaza wamepanda miti ya matunda kama vile miembe,machungwa,mipera na mipapai.Lakini pia bustani ya mbogamboga kwa lengo la kukabiliana na janga la ukame lakini pia kuboresha lishe ya wanafunzi na kupendezesha madhari ya shule yao.Girl guide pia walitoa shukrani kwa TGGA kwa kuwawezesha fedha kwaajili ya ununuzi wa miche ya matunda ,lakini pia walitumia nafasi hiyo hiyo kuwashukuru wakala wa misitu (TFS) kwa kuwapatia miche ya kivuli.

vilevile kwenye risala yao pia walibainisha changamoto mbalimbali ambazo wamekuwa wakikutana nazo ambazo hukwamisha ndoto zao ni kama vile,ukosefu wa miundombinu ya maji safi(LUWASA) ambayo inapelekea jitihada zao za kuanzisha klabu za kijani kukwama,kwani kwa sasa wanategemea sana maji ya mvua au kuteka maji kutoka maeneo ya mbali,jambo linalohatarisha ulinzi na usalama kwa wasichana hao.

Mwisho mgeni rasmi katika tukio hilo la upandaji wa miti Ndg,Moses Mkoveke alipata nafasi ya kupanda mti,vile vile alitumia nafasi hiyo kumpongeza mwalimu mkuu washule ya sekondari Angaza kwa juhudi ambazo anazifanya katika kuhakikisha mazingira ya shule hiyo yanakuwa mazuri.Lakini pia alipata nafasi ya kuongea na wanafunzi waliohudhuria katika tukiko hilo kwa kuwasisitiza waendelee kupanda miti mpaka pale watakapo ishiwa na nguvu.Mkoveke pia alitumia nafasi hiyo kuwaalika Girl guide katika siku ya wanawake, ambayo kimkoa inafanyika Nachingwea siku ya tarehe 3/4 mwezi wa tatu,hivyo wafike na kupeleka bidhaa zao katika siku hiyo wa wanawake kimkoa wa Lindi.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA JANUARI 2023 December 15, 2022
  • Tangazo kwa umma: Uuzaji wa dawa muhimu kwa binadamu November 30, 2022
  • Kuitwa kwenye usaili November 08, 2022
  • TAARIFA KWA UMMA: MAPOKEZI YA FEDHA ZA MIRADI October 03, 2022
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • KAMATI YA LAAC YAPONGEZA UONGOZI NA WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI LINDI PAMOJA NA KUTOA MAELEKEZO KWA TAMISEMI

    March 23, 2023
  • SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SIKU YA KUJIKUMBUSHA WAJIBU PAMOJA NA MAJUKUMU YETU . RC-TELACK

    March 08, 2023
  • MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MANISPAA YA LINDI YAFANA.

    March 06, 2023
  • MANISPAA YA LINDI YAPOKEA PIKIPIKI 22 KUTOKA KWA DKT. SAMIA SULUHU HASSAN KWAAJILI YA MAAFISA KILIMO

    March 13, 2023
  • Ona Yote

Video

Tamko la Mkuu wa Wilaya ya Lindi kuhusu zahanati ya Mnali
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa