Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Ndugu Jomaary Mrisho Satura akiwa kwenye kikao na walimu wa shule za Manispaa ametoa pongezi kwa walimu hao kwa juhudi wanazozifanya huku akiwaomba kufanya kazi kwa bidii, ufanisi na nidhamu ya hali ya juu kuhakikisha ufaulu wa wanafunzi ukiongezeka zaidi. Pia katika kikao hicho Mkurugenzi ametoa ahadi ya kukarabati baadhi ya shule ikiwemo shule ya sekondari Mchinga,shule ya msingi Ruaha na Makumba na kupaka rangi baadhi ya shule.
Afisa Utumishi wa Manispaa (wa pili kutoka kushoto) Ndugu Kihanza amewaasa walimu hao kuimarisha mawasiliano baina yao walimu na ngazi ya juu ili kuleta urahisi katika utatuzi wa changamoto kwa haraka. Vilevile amewataka walimu kuwa na nidhamu ya kazi na malengo kwa taasisi yao. Amewakumbusha kuzingatia uimarishaji wa mwili kwa kuzingatia usafi na ulaji wa vyakula bora ili kuepusha magonjwa na kwa upande wa wanafunzi kuwafanyisha mazoezi ya viungo asubuhi (Mchakamchaka).
Pia, Walimu walifanya majadiliano ya jinsi gani ya kutatua changamoto zinazowakabili wanafunzi na walimu mashuleni ikiwepo utafutaji wa suluhu juu ya kutokuwepo kwa kambi kwa madarasa yenye mitihani ya Taifa ili kusaidia ufaulu kwa wanafunzi ambapo Mtaaluma wa elimu amewataka walimu kutumia muda wa kazi vizuri kwa wanafunzi.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa