Katika kuendelea kutekeleza maelekezo ya Serikali ya kila halmashauri kutenga asilimia kumi (10%) ya mapato yake ya ndani, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imeviwezesha kiuchumi vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu.
Katika mwaka 2019/2020, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ilitenga Tshs 102,793,499.97 kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vya Wanawake, Vijana na watu wenye ulemavu.Aidha ,ilitenga Tshs 59,293,500.00 kwa ajili ya kukopesha kikundi cha Mamalishe Sabasaba, pesa ambazo ndizo zilizotumika kujenga jengo la Mamalishe Sabasaba Manispaa ya Lindi kama linavyoonekana kwenye picha hapo chini:
Katika mwaka wa fedha 2020/2021, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imetenga Tshs 208,224,000.00 kwa ajili ya kuvikopesha vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye ulemavu. Aidha, hadi kufikia 31 Oktoba, 2020 jumla ya Tshs 83,292,500.00 zilikuwa zimeshakopeshwa kwa vikundi 14 vikiwemo vitano (5) vya Wanawake, sita (6) vya Vijana na vitatu (3) vya watu wenye ulemavu.
Kikundi cha Mamalishe Sabasaba kinaundwa na Wanawake kumi na nne (14) ambao wote ni Mamalishe.Kikundi hiki kimetambuliwa na Halmashauri na kupewa cheti cha utambuzi chenye Na.LMC/CBO/946. Mara baada ya kuomba mkopo kutoka Halmashauri na kupatiwa pesa hizo, wamezitumia kujenga jengo lenye jumla ya vyumba kumi (10), kuweka milango na madirisha ya vyuma (Grill), kutengeneza mfumo wa maji taka pamoja na mfumo wa umeme na kununua samani (viti 60 na meza 10) vyote vya plastiki. Aidha, wameshailipa TANESCO gharama zote za kuingiza umeme katika jengo hilo.
Lengo la kikundi cha Mamalishe Sabasaba kuchagua kujenga jengo hilo ni kuboresha mazingira ya kufanyia shughuli zao za kupika na kuuza vyakula.Hii itapekelekea wananchi wengi na wa aina zote kuhamasika kupata huduma mahali hapa na hatimaye kuwawezesha kujiongezea mapato yao yatakayosaidia kuinua hali za maisha katika kaya zao.
Baada ya uzinduzi wa jengo hilo, Katibu tawala wa Wilaya ya Lindi ndugu Thomas Safari na kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi ndugu Baptista Kihanza waliwaasa Mamalishe wote watakaopata fursa ya kupata vyumba katika jengo hilo kuwa waangalifu katika matumizi ya jengo hilo na kulitunza ili vizazi vijavyo viweze kulitumia pia. Aidha Mamalishe walishukuru sana kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwa kuwapatia fursa hiyo ambayo ni adhimu kwao na kuahidi kulitunza jengo hilo.
Baadhi ya Mamalishe wakiwa na nyuso za furaha katika uzinduzi wa Jengo la Mamalishe Manispaa ya Lindi.
Muonekano wa ndani wa moja ya chumba cha jengo la Mamalishe Manispaa ya Lindi.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa