Baraza la Madiwani la tarehe 20.02.2021, limefanyika katika ukumbi wa St. Andrea Kagwa ambapo taarifa mbalimbali za Maendeleo ya Manispaa ya Lindi za robo ya pili ya mwaka 2020/2021 zimejadiliwa na wajumbe wa Baraza (Madiwani), Wakuu wa idara na vitengo,viongozi wa kamati ya ulizi na usalama, pamoja na Wataalam wa Taasisi mbalimbali kama TARURA, RUWASA, TANESCO, SWISSAID na Shirika la bima ya afya walioalikwa ili kutoa ufafanuzi wa taarifa mbalimbali sambamba na kujibu maswali mbalimbali ya wajumbe.Maswali mengi yalielekezwa katika Taasisi mbili ambazo ni TARURA na RUWASA ambapo wajumbe waliwasilisha changamoto za barabara na maji zinazopatikana katika maeneo yao. Aidha, maswali yote yalijibiwa na wataalam wa taasisi hizo na kuendelea kuahidi kuonyesha ushirikiano wa juu pale ambapo watahitajika.Baadhi ya picha za wataalam hao wakati wakijibu hoja za wajumbe ni kama zinavyoonekana hapo chini:
Meneja wa TARURA mtama akijibu hoja za wajumbe mbalimbali wa jimbo la Mchinga.
Mtaalam kutoka RUWASA akijibu hoja zinazohusiana na maji zilizowasilishwa na wajumbe.
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Lindi mhe. Frank Magali alitoa pongezi kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi na timu yake kwa ujumla kwa kazi nzuri wanayofanya katika nyanja mbalimbali. Pongezi nyingi zilienda kwa idara ya elimu ambapo Maafisa elimu walipongezwa kwa kuboresha elimu na kuongeza ufaulu wa wanafunzi. Aidha, Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi ndg. Jomaary Satura aliendelea kusisitiza kudumisha umoja na ushirikiano baina ya watumishi kwani maendeleo ya Manispaa ni jukumu la kila mtumishi na aliendelea kusema kwamba watumishi wote wanajenga nyumba moja kwa hiyo suala la ushirikiano halina budi kuhimizwa.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa