• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

WAJASIRIAMALI MANISPAA YA LINDI WAPIGWA MSASA ELIMU YA UJASIRIAMALI.

Imetumwa: March 13th, 2025

Wajasiriamali Halmashauri ya Manispaa ya Lindi wamepata mafunzo kuhusu Elimu ya ujasiriamali ili kuweza kuongeza thamani ya bidhaa na Huduma wanazozitoa lakini pia kuwa na namna Bora ya kujiongezea vipato vyao.

Elimu hiyo imetolewa leo  machi 13 , 2025 Kwa wajasiriamali pamoja na viongozi wa VIKOBA Manispaa ya Lindi katika ukumbi wa mikutano Lindi Sekondari.

Akiongea na washiriki hao mara baada ya ufunguzi wa mafunzo hayo mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva amesisitiza washiriki hao kuwa na umoja na mshikamano katika vikundi vyao.

Aidha amewaomba kuchangamkia fursa ya mikopo 10% inayotolewa na Halmashauri Kwa Vijana, Wanawake na wenye ulemavu, mikopo ambayo haina riba.

Naye Mkuu wa idara ya maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Peter Nambunga amewaomba washiriki hao kuwa na ushirikiano katika masuala mbalimbali kwenye vikundi vyao, lakini pia kuhakikisha wanakuwa na vitambuliaho vya wajasiriamali ili waweze kutambulika wao na shughuli zao.

Akitoa Elimu ya umuhimu wa VIKOBA Kwa washiriki hao Afisa maendeleo ya Jamii kata ya Kitumbikwela January kazimoto amesema VIKOBA husaidia kutatua matatizo ambayo mtu mmoja au familia isingeweza kuyatatua, lakini pia husaidia kuleta maendeleo Kwa Jamii hasa zenye hali duni, matumizi Bora ya rasilimali pamoja na kuleta upendo, mshikamano na amani katika Jamii.

Nao washiriki wa mafunzo hayo wameipongeza idara ya maendeleo ya Jamii Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Kwa kuandaa mafunzo hayo muhimu kwao ambayo yanakwenda kuwasaidia katika kukuza shughuli na biashara zao.

Licha ya kupata Elimu ya ujasiriamali washiriki hao pia wamepata kujifunza kuhusu Elimu ya uimarishaji na uundaji wa vikundi, Elimu ya utunzaji wa kumbukumbu, Elimu ya uongozi, Elimu ya masoko na leseni, matumizi sahihi ya mikopo na uendeshandaji wa vikundi, fursa za kibenki pamoja na elimu ya msaada wa kisheria kutoka Kwa dawati la msaada wa kisheria (Mama Samia Legal Aid Campaign).

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa