• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

NAIBU WAZIRI MALIASILI NA UTALII AFIKA ENEO LA TENDAGURU NA KUELEZA MIKAKATI YA SERIKALI YA KULITANGAZA NA KULIENDELEZA

Imetumwa: July 21st, 2021

Naibu waziri wa Maliasili na Utalii mhe. Mary Masanja amefanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali yenye vivutio vya utalii mkoani Lindi.Katika ziara yake ya tarehe 21/07/2021 Mhe. Mary Masanja ametembelea eneo la kihistoria duniani la Tendaguru lililopo katika kata ya Mipingo, Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.Eneo la Tendaguru ndipo yalipogunduliwa mabaki ya mijusi ya kale (Dinasours) mnamo mwaka 1908 na Injinia waKijerumani aitwaye B. Sattler alipokuwa anafanya utafiti wake wa Sayansi ya miamba.Baada ya kuripoti mabaki hayo kwa wanasayansi wa mambo ya kale huko Berlin, nchini Ujerumani, Taassisi na Makumbusho ya Malikale ya Ujerumani ilileta wataalamu kwa ajili ya kufanya utafiti katika eneo hilo. Utafiti ulifanyika kwa kipindi cha miaka minne kuanzia 1909-1913 na mabaki ya mijusi yaliyopatikana yalisafirishwa hadi Ujerumani.

Mhe. Mary Masanja amempongeza mbunge wa jimbo la Mchinga Mhe. Salma Kikwete kwa kusimama kidete bungeni na kulizungumza suala la mabaki ya mjusi mkubwa duniani yaliyogunduliwa katika eneo la Tendaguru lilnalopatikana jimboni kwake.Mhe. Naibu waziri amesema adhma ya Serikali ilikuwa ni kusafirisha mabaki hayo kutoka huko Berlin na kuyaleta hadi katika eneo lenye chimbuko la asili yake (Tendaguru) lakini kutokana na sababu za msingi zilizotolewa, imeshindikana kusafirisha mabaki hayo.Serikali chini ya wizara ya Maliasili na Utalii imedhamiria kulitangaza na kuliendeleza eneo hilo la historia ya Taifa na Kimataifa.

Aidha, Naibu Waziri amewaagiza viongozi wa Wilaya ya Lindi na viongozi wa Manispaa ya Lindi kulilinda eneo hilo kwani baadhi ya wananchi wa jamii za kifugaji wameanzisha makazi katika maeneo yanayolizunguka eneo hilo la kihistoria."TFS mpo hapa na nawaagiza kwamba yeyote atakayethubutu kuingiza mifugo yake katika eneo hili basi achukuliwe hatua kali", alisema Mhe. Mary Masanja.Pia mhe. Naibu Waziri amewaasa wananchi wa mkoa wa Lindi Kwa ujumla kuchangamkia fursa hiyo ya serikali ya kuipa kipaumbele kanda ya kusini kwa sababu ina maeneo mengi ya kihistoria na kiutalii.Wananchi wamehimizwa kudumisha utamaduni wao na kuandaa mazingira yakayochochea utalii endelevu.

Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Salma Kikwete na Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga wameishukuru wizara ya Maliasili na Utalii na Serikali kwa ujumla kwa mikakati hiyo ya kulitambua, kulitangaza na kuliendeleza eneo hilo la Tendaguru pamoja na maeneo mengine yaliyopo katika mkoa wa Lindi.Pia  wameiomba serikali kuwashirikisha wananchi kwa ukaribu katika mikakati hiyo kwani wao ndio waliopo karibu sana na maeneo hayo ya kihistoria na kitalii.

Aidha aliyekuwa Mbunge wa viti maalum mwaka 2015-2020 Bi. Riziki Saidi Lulida aliyejipa jina la Mama mjusi amempongeza Mhe. Mary Masanja kwa kuwa kiongozi wa kwanza wa ngazi ya juu ya serikali kutembelea eneo la Tendaguru na kumsifu kwamba anafanya kazi kwa kuendana na kasi ya Mhe.Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Pia Bi. Lulida amemuomba Mhe. Naibu waziri kwamba vijana wanaozunguka maeneo ya kitalii wawezeshwe kuunda Village Game Skauti ambayo itawasaidia vijana kujihusisha na shughuli za kiuchumi kama kupatiwa mizinga kwaajili ya kufuga nyuki.Vijana hawa watakuwa walinzi wazuri wa maeneo ya kiutalii wanapokuwa wanendelea na shughuli zao za ufugaji wa nyuki.

Kaimu Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Ndg. Baptista Kihanza akipanda katika mlima Tendaguru yalipogunduliwa mabaki ya mjusi mkubwa duniani.


Mbunge wa viti maalum (2015-2020) Bi. Riziki S. Lulida akitoa historia ya Tendaguru na kumshukuru Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa kulitembelea eneo hilo la kihistoria.





Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa