• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MIAKA 22 (1999 - 2021) YA KUMBUKUMBU YA KIFO CHA HAYATI MWL. JULIUS KAMBARAGE NYERERE

Imetumwa: October 14th, 2021

Hayati Mwl.Julius Kambarage Nyerere alizaliwa mwezi machi 1922 Butiama Tanganyika (Tanzania kwa sasa) na alikufa akiwa na miaka 77,na kuzikwa katika kijiji cha Mwitongo Butiama Kaskazini mwa Tanzania. Alifanikisha uhuru wa Tanganyika 1961 dhidi ya ukoloni wa Muingereza.

Tanganyika ilipata uhuru mwaka 1961 chini ya uongozi wake bila kumwaga damu , jambo alilosifiwa kama mmoja wa viongozi waliokua wana Imani ya kijamaa.Mwl.Nyerere alikua akiamini katika falsafa ya Ujamaa na kujitegemea. Hayati mwl. Nyerere alifanya hotuba mbalimbali katika mikutano ya ndani na nje ya nchi wakati wa uongozi wake na hata baada ya kustaafu. Mwalimu Nyerere atakumbukwa kama Baba wa Taifa katika mambo makuu mbalimbali aliyoyafanya.

Yafuatayo ni mambo aliyopenda kuyasisitiza katika hotuba zake enzi za uhai wake:

  • Ukabila - Suala la ukabila ni jambo nyeti ambalo nyerere aligusia katika hotuba nyingi alizowasilisha. Aliwahi kusema ''nilikutana na mama mmoja akaniambia alikua akifanya kazi jumuiya ya afrika mashariki, na sisi watu wa uganda tulikua tunajuana kwa makabila yetu , watu wa kenya walikua wakijuana kwa makabila yao, huyu mkikuyu, huyu mluhya. Lakini sisi watanzania hatujui makabila ya watu, nikawambia mama ni wakati huo, sasa hivi watanzania wanataka kujua makabila yao, ya nini, mnataka kutambika? Majirani zetu waalikua wanaiga kutoka Tanzania, sasa bila haya na sisi tunataka kuulizana makabila? Mwalimu Nyerere katika hotuba yake ya mkutano mkuu wa CCM 1995.
    Nyerere alikemea suala la ukabila kila wakati alipopata nafasi ya kuzungumza na hakutaka kabisa kuwe na maswali kama wewe ni kabila gani? N katika hilo alifanikiwa kwa kiasi kikubwa, si kwa kawaida nchini Tanzania kuulizana kuhusu masuala ya ukabila.
  • Dini -  Jambo ambalo alisisiza sana katika hotuba zake, hasa kuwaasa viongozi wasitafute uongozi kwa kutumia dini.Aliwahi kusema ''mambo haya ya kuchochea chuki za dini yakianza na tukayapa nafasi hayana simile, ni ikifika wakati yakashika kasi hakuna wa kuzuia''.
  • Ujinga, maradhi na Umaskini - Mwalimu Nyerere alisisitiza juu ya mambo haya makuu matatu, kama na aliongeza pia kama Tanganyika na baadae Tanzania itafanikiwa kuyamaliza basi itakua miongoni mwa nchi itakayoendela zaidi duniani.Katika suala la kupinga umasikini Mwal. Nyerere aliwahi kusema ''nchi hii ni bado ya wakulima na wafanyakazi, hatuwezi kuwa nchi ya watu wenye kudai na kudai, nawaomba ndugu zangu watanzania hatujalemaa sana, lakini kilema kipo, viongozi wetu wanadai na kudai tuu, watu ni maskini, wachache hao wana nguvu ya kuongoza nchi hii ndio wanaodai tuu''.
  • Uongozi -  katika suala la uongozi, maadili ya uongozi ni jambo aliloliweka mbele sana, miongoni mwao ni viongozi ambao wanaweza kukidhi matarajio ya watanzania. Nukuu mojawapo ya hotuba yake akizungumzia uongozi ni ''watanzania wanataka mabadiliko, wasipoyapata ndani ya CCM, watayapata nje ya CCM, inatakiwa ukiulizwa swali kwamba huyu atapiga vita rushwa? Jibu litoke ndani ya moyo, nchi yetu ni maskini bado haijawa ya matajiri hivyo tunataka tuendelee kushughulika na umaskini wetu na matatizo ya wananchi, tunataka nchi yetu ipate kiongozi safi''. 
  • Muungano - katika vitu ambavyo alikua akitamani sana kufanya ni kuunganisha nchi za Afrika mashariki, na kuwa na uongozi wa pamoja, ingawa hakufanikiwa katika hilo, alifanikiwa katika kuunganisha Tanganyika na Zanzibar mwaka 1994. Nukuu ''matumaini yangu, ilikua kuunganisha nchi hizi za Afrika mashariki na kuwa muungano mmoja, kwa upande wa Zanzibar niliongea na Karume, akasema niko tayari ita watu wa magazeti sasa hivi, nikamwambia tufanye taratibu na tukafanikiwa. Kwa Afrika mashariki tungekua na serikali tatu za kila nchi na serikali ya muungano yani ya tanganyika na muungano''.

Hayo ni baadhi ya mambo aliyopenda kusisistiza sana Hayati Mwl. Julius Kambarage Nyerere katika hotuba zake. Watanzania tukiwa tunaadhimisha miaka 22 ya kifo cha baba wa Taifa tunapaswa kuishi falsafa zake na kuyaenzi yote mazuri aliyofanya. Hakika tutamkumbuka daima shujaa wa Taifa letu.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa