• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MAKALA TASAF (PART 1): TASAF YAWA MUHIMILI MKUBWA KATIKA KUBORESHA MAISHA YA KAYA YANGU

Imetumwa: May 26th, 2018

Bi Afa Mohamed Masudi ni mama mwenye umri wa miaka 60 na ni miongoni mwa kaya 2468 zinazonufaika na Mpango wa TASAF III wa kunusuru kaya maskini sana katika Manispaa ya Lindi. Bi Afa anaishi katika Kata ya Mtanda, Mtaa wa Mtanda Juu. Mama huyu amesajiliwa kwa namba PSSN-LMC-02438-1 na amekuwa akinufaika na mpango huu wa kunusuru kaya maskini sana toka mwaka 2013 ambapo ameshapokea ruzuku kwa awamu 31.

Kaya ya Afa Mohamed Masudi ina jumla ya watu saba (7) ambapo miongoni mwao watoto ni watatu (3) na ambapo watoto wawili wanasoma shule ya msingi Mtanda darasa la pili na la nne na mmoja anasoma kidato cha kwanza shule ya sekondari Angaza. Kaya hii ina watu wazima  wanne (4) ambao ni wategemezi wa Bi Afa.  

Kabla sijajiunga na Mpango wa TASAF wa Kunusuru Kaya Maskini sana, hali yangu ya maisha ilikuwa ngumu sana hasa katika upatikanaji wa chakula kwani tulikuwa tukila mlo mmoja na mara chache sana milo miwili. Aidha uwezo wa kwenda hospitalini ulikuwa mdogo kutokana na ukosefu wa fedha ikiwa ni pamoja na kushindwa kuwagharamia wajukuu wangu mahitaji ya shule kama vile sare za shule, madaftari, kalamu na viatu. Mara nyingi wajukuu wangu walikuwa hawaendi shule kwa kukosa madaftari na kalamu. Makazi yangu nayo pia yalikuwa duni sana maana nilikuwa nikiishi katika nyumba iliyoezekwa kwa makuti na kusiribwa kwa tope na sakafu ya udongo. Kwasasa sasa toka nijiunge na TASAF maisha yameboreka kwani ninamudu kununua chakula chakutosha na hata nikienda kukopa dukani ninakopeshwa. Pia ninamudu kulipia gharama za shule kwa wajukuu wangu, nimejiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na nimeboresha nyumba yangu kwa kuweka bati na kuisakafia. Maelezo haya aliyatoa Afa Mohamed Masudi.                                                                                                                       

Kaya ya Afa Mohamed Masudi imekuwa ikipokea ruzuku ya kunusuru kaya maskini toka mwaka 2013 ambapo hadi Machi 2018 amepokea mara 31. Bi Afa alianza kupokea Tsh 28,000.00 na kwasasa anapokea Tshs 56,000.00. Aidha kutokana na ruzuku ambayo imekuwa ikipokelewa na kaya hii pamoja na ujira wakati wa kazi za ajira ya muda, Bi Afa Mohamedi amemudu kuwanunulia wajukuu wake vifaa vya shule na kuboresha nyumba yake kwa kuezeka kwa bati. 

“Kutokana na mimi kuwa kwenye mpango pamoja na kuongezeka kwa ruzuku, nimemudu kuanzisha Biashara ya kununua na kuuza mkaa, nimenunua mbuzi mmoja kwa Tshs 50,000.00 ambaye kwa sasa ana mimba”, alisema Afa Mohamed Masudi.

Wakati wa mahojiano, Afa Mohamedi Masudi alisema kuwa amemudu kununua mbuzi mmoja wa maziwa na kuboresha biashara yake ya kununua na kuuza mkaa ambayo inamwingizia Tsh 3,000.00 kama faida kwa kila kiroba. Kipato anachopata kutokana na kuuza mkaa pamoja na mazao mengine ya kama vile mtama hutumika kuisaidia kaya hii kujikimu wakati ikiendelea kusubiria pesa za Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini.

“Kipato ninachopata kwasasa kutokana na Biashara zangu binafsi kinanisaidia kujikimu kwa muda wote ambao kunakuwa hakuna malipo kutoka TASAF; ama kweli TASAF imekuwa muhimili mkubwa katika kuinua maisha ya kaya yangu”, alisema Afa Mohamed Masudi.

Wakati wa mahojiano, Afa Mohamed Masudi alisema ana vitu vingi vya kujivunia ila anajivunia zaidi kule kuwa na uhakika wa lishe (milo mitatu) kwa siku, uhakika wa matibabu kwakuwa wanakaya wana vitabulisho vya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) na anauhakika wa kuwalipia wajukuu wake gharama za shule.  

Bi Afa Mohamed Masudi, alisema kuwa anawashauri wale wote ambao wapo kwenye mpango wa Kunusuru kaya maskini wasibweteke kwa kuitegemea TASAF peke yake kwani kuna siku itajiondoa katika ufadhili wake. Hivyo aliwataka wajishughulishe na shughuli zingine za uzalishaji mali kama vile kilimo, ufugaji wa mifugo na biashara ndogo ndogo. Aidha aliishukuru Serikali kwa kuzisaidi kaya maskini kuinua hali zao za maisha. Pia aliitaka kuendelea kuzisaidia kaya zingine ambazo ni maskini ili nazo zijikwamue kimaisha.

Mipango ya baadaye ya Bi Afa Mohamed Masudi ya maendeleo ili kaya yake iondokane na umaskini ni pamoja na;

  • Kuongeza biashara ya kuuza mkaa
  • Kuongeza shamba la mazao ya nafaka
  • Kuboresha makazi ya kaya kwa kujenga nyumba ya tofali
  • Kuongeza mifugo kama vile kuku

Taarifa hii imeandaliwa na Ofisi ya TASAF Manispaa ya Lindi

Mei, 2018


Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa