• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

CRDB BANK YAKABIDHI MIFUKO MIA MOJA YA SARUJI KWA SHULE YA SEKONDARI LINDI WASICHANA.

Imetumwa: March 10th, 2025

Benki ya CRDB imekabidhi mifuko mia moja  ya saruji Kwa shule ya Sekondari Lindi Wasichana iliyopo kata ya Kilangala Jimbo la Mchinga Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, kwaajili ya Ujenzi wa uzio shuleni hapo. 

Akiongea na wanafunzi wa shule hiyo  mara baada ya kukabidhi mifuko hiyo meneja wa CRDB kanda ya Kusini Bwana Denis Mwoleka amesema mifuko hiyo ya saruji  ni muendelezo wa mambo mbalimbali ambayo yanafanywa na benki hiyo katika kurudisha Kwa Jamii.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mhe. Victoria Mwanziva ambaye pia alikuwa ni mgeni rasmi katika Hafla hiyo ameishukuru benki ya CRDB Kwa kutoa mifuko hiyo ya saruji lakini pia amewaomba wanafunzi katika shule hiyo kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili waweze kufanya vizuri kwenye masomo yao. 

Akipokea mifuko hiyo ya saruji kutoka kwa meneja wa CRDB kanda ya Kusini Mstahiki Meya wa Manispaa ya Lindi Mhe. Frank Magali ameishukuru benki hiyo Kwa msaada huo ambao unakwenda kusaidia katika Ujenzi wa uzio katika shule hiyo.

Sambamba na hilo Magali ameishukuru serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mhe. Dkt, Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kwa kazi kubwa na nzuri anayoifanya hasa Katika Manispaa ya Lindi Mkoa wa Lindi na taifa Kwa ujumla.

Lakini pia ametumia nafasi hiyo kumshukuru Mbunge wa Jimbo la Mchinga Mhe. Salma Rashidi Kikwete Kwa kazi anayoifanya katika kuhakikisha Jimbo hilo linapata maendeleo hususani ni kata ya Kilangala.

 Pamoja na hayo naibu mstahiki Meya Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ametoa wito kwa wazazi na walezi katika kata hiyo kuweka utaratibu wa kufanya usafi kuzunguka mazingira ya shule hiyo.

katika hatua nyingine katibu wa mbunge Jimbo la Mchinga Abdallah Mkokoi Kwa niaba ya mbunge wa Jimbo hilo ametoa kiasi Cha fedha shilingi laki tano Kwa Wanafunzi wa shule hiyo kwaajili ya kununua futari kwenye mwezi huu wa mfungo.

Ikumbukwe kuwa tarehe 09 Agosti 2024  benki hiyo chini ya meneja wake Kwa kanda ya Kusini ilikabidhi viti na meza 40 shuleni hapo ikiwa ni katika kusaidia kukuza na kuendeleza sekta ya Elimu .

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa