• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

BARAZA LA MADIWANI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LIINDI.

Imetumwa: May 20th, 2023

Baraza hilo limefanyika ukumbi wa DDC Manispaa ya Lindi mei 20,2023 likiongozwa na mstahiki meya wa Manispaa ya Lindi Mhe Frank Magali pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Manispaa ya Lindi Juma Mnwele, lakini pia lilipata kuhudhuriwa na mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga , pia mwenyekiti wa CCM wilaya ya Lindi mjini Bakari Ali Bwatamu , vile vile madiwani wa kata zote zilizopo Manispaa ya Lindi walihudhuria, sambamba na wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya Lindi pamoja na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.

Ajenda mbalimbali zilipata kujadiliwa kwenye baraza hilo,ikiwemo maswali sita ya papo kwa papo kutoka kwa madiwani yalipata kuwasilishwa mbele ya mwenyekiti wa baraza hilo ambaye ni mstahiki meya wa Manispaa ya Lindi na kupata kujibiwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Juma Mnwele.

Katika hatua nyingine mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe Shaibu Ndemanga ambaye pia alipata kuhudhuria kayika baraza hilo, aliwapongeza wajumbe wa baraza hilo ambao ni madiwani kwa kazi kubwa wanazo zifanya kwenye kata zao,  lakini pia aliwapongeza madiwani wote kwa ushirikiano mkubwa wanao ufanya katika shughuli mbalimbali  hususani ni matukio maalum kama vile mwenge wa uhuru.

Aidha, Mhe .Ndemanga aliwapa pole madiwani wote kwa kumpoteza diwani wa mwenzao wa viti maalum katika kata ya Mipingo  lakini pia aliwapongeza madiwani wote kwa kuchukua hatua za haraka za kujaza pengo lake. Vile vile Mhe. Ndemanga alitoa taarifa kuhusu wanyama waharibifu ikiwemo tembo kwenye eneo la Milola , Manispaa ya Lindi pamoja na maeneo mengine ya Halmashauri ya Mtama, taarifa hiyo ni hatua zilizo chukuliwa na serikali kuongeza  askari wanyama pori kutoka askari wawili (2) ambao walikuwepo mpaka kufikia askari sita(6), ambao tayali wameshapatiwa mafunzo maalum, hata hivyo serikali imeahidi kuongeza zaidi askari wanyama pori lakini pia  serikali imetoa gari maalumu mpya mpya kwaajili ya kurahisisha  utendaji kazi wa askari hao vile vile serikali imetenga bajeti kwaajili ya upatikanaji wa mafuta , sambamba na hilo serikali imejenga kituo maalum  cha askari wanyama pori eneo la Milola kwaajili ya kudhibiti wanyama pori

Lakini pia  alichukua nafasi hiyo kutoa pole kwa wakazi wa Lindi ambao wameathirika  kutokana na wanyama pori. Katika hatua nyingine Mhe. Ndemanga alisisitiza wajumbe wa baraza hilo kusimamia suala la upatikanaji wa mapato katika halmashauri yetu.

Mwisho mstahiki meya wa Manispaa ya Lindi Mhe. frank Magali amesisitiza wajumbe wa baraza hilo kuchakikisha wakazi wa Manispaa ya Lindi wana changamkia fursa ya viwanja 3200 vitakavyo  tangazwa kuuzwa katika eneo la Mto mkavu kuelekea Mbanja kwani vianja hivyo ni mali ya wananchi wote na wanatakiwa kuchangamkia fursa ya viwanja hivyo. Lakini pia kuhakikisha wanafuatilia suala la upatikanaj wa mapato katika vijiji na mitaa yao. 

Sambmba na hilo mstahiki meya wa Manispaa ya Lindi alimpongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mhe. Dkt . Samia Suluhu Hassan, kwa mambo  yote ya kimaendeleo anayo tuletea ndani ya Manispaa ya Lindi lakini pia mkoa wa Lindi kwa ujumla ikiwemo mradi wa ujenzi wa chuo cha oil and gas mradi ambao utatumia Bilioni 80 mradi huo upo katika eneo la Kikwetu pamoja na ujenzi wa chuo kikuu cha Dar es salaam ndaki ya kilimo ujenzi ambao unategemewa kujengwa kufikia mwezi wa sita mwaka huu katika eneo la Ngongo Manisapaa ya Lindi.


Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa