• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

ZIARA YA KIKAZI YA WAZIRI MKUU MHE. KASSIM MAJALIWA (MB) KUKAGUA MIRADI MBALIMBALI NDANI YA MKOA WA LINDI.

Imetumwa: October 5th, 2021

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa afanya ziara Mkoa wa Lindi leo tarehe 05.09.2021 ambapo kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ameweza kutembelea eneo la mizani Mnazimmoja,Tenki la maji Mitwero na kufanya ufunguzi wa gari la maji taka la LUWASA, na kutembelea eneo la mradi mkubwa wa gesi (LNG). Katika ziara yake Ndani ya Manispaa ya Mhe. Majaliwa amekagua kituo cha mizani cha Mnazi Mmoja na kutoa maagizo kwa meneja wa TANROADS mkoa wa Lindi kufanya maboresho ili kuongeza ufanisi wa mizani hiyo na kurahisisha uingiaji na utokaji wa magari. Mhe. Mjaliwa amesema Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ametoa fedha zaidi ya bilioni 2.469 kwa ajili ya kufanya maboresho katika vituo 42 vya mizani kikiwemo kituo hicho cha Mnazi Mmoja.Pia alitembelea eneo la Likong'o ambapo utatekelezwa mradi mkubwa wa gesi (LNG) na kupata wasaa wa kuongea na wananchi na kutoa rai kwa viongozi na wananchi wa Manispaa ya Lindi kujiandaa kikamilifu kwani mradi huo upo mbioni kutekelezwa.‘’Tunaenda kwa spidi kubwa ili mradi huu uweze kutekelezwa ikiwemo kuwa na majadiliano  na kampuni zile zinazounda kitu kimoja cha kuja kujenga mradi huu na kampuni zote tatu zinahusika na mradi huu tumefikia hatua sasa tumefanya maandalizi ya kukaa pamoja na wataalamu wetu walikuwa wanakamilisha kwenda kuanza majadiliano hii ni hatua tu ya kuelimishana kwamba sisi watanzania tunataka kiwepo  hiki ili wananchi wetu waweze kunufaika na tunawashawishi wakubali kwani wanania ya kuja kuwekeza’’, alisema Mhe. Majaliwa.

Aidha, Mhe. Majaliwa amewaambia wananchi wa Manispaa ya Lindi kujiandaa na ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan ambaye atazindua utekelezaji wa mradi huo. Aliendelea kuwaambia wananchi hao kuwa wawe tayari kwa mradi kwani hakuna mashaka na yeye anasafisha njia ili Mheshimiwa Rais aweze kuja.Katika kuendelea kuongea na wananchi wa Manispaa ya Lindi Mhe. Majaliwa alitoa maagizo kwa Mkurugenzi wa TPDC ambapo amempa wiki moja kuhakikisha anachonga barabara kuelekea eneo la mradi. Mhe. Majaliwa alimpongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Ndg. Juma Ally Mnwele kwa kazi nzuri iliyofanyika ya ujenzi wa barabara mbalimbali ndani ya Manispaa na kumuagiza  kuanza mara moja ujenzi wa barabara ya Rutamba.

Pia Mhe. Majaliwa amewatoa hofu wananchi kuhusu suala la ajira kwenye mradi huo ambapo alisema moja ya lengo la majadiliano na wawekezaji ni kuhusu ajira kwa wa maeneo ya jirani na eneo la mradi na Lindi kwa ujumla.Ambapo ili kupanua wigo wa ajira hizo kutakuwa na mitaala ya mafunzo juu yauchakataji gesi kwenye vyuo vya VETA.Kupitia mradi wa gesi maendeleo makubwa yatafanyika ikiwemo ukarabati wa uwanja wa ndege wa Kikwetu na uhakika wa umeme masaa 24 wakutosha na kwa bei nafuu ili kuhakikisha kila mwananchi anavutia umeme nyumbani kwake.Vilevile kwenye sekta ya maji  Waziri amesema ‘’Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan ametoa billioni mbili pointi tano ili kuweza kufanya uendelezaji miradi ya maji’’.

Aidha, Waziri  Mkuu amewahamasisha wananchi kuwekeza kwenye mambo mbalimbali yenye kuleta tija lakini pia kusapoti mradi huo ili kuleta mzunguko wa fedha.Amewashauri pia kufanya uwekezaji wa kujenga hoteli ili kuwafanya wawekezaji na wafanyakazi kulala Lindi na si sehemu nyingine.                                                                            

 

Mbunge wa Jimbo la LIndi mjini Mhe. Hamida Abdallah akiwasalimia wananchi wa eneo la Likong'o

 waliojitokeza katika ziara ya Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb).

Gari jipya la Majitaka litakalotumika ndani ya Manispaa ya Lindi



Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa