• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

UJIO WA DKT KIKWETE KUJA KUFUNGUA FURSA MBALIMBALI MKOA WA LINDI

Imetumwa: January 9th, 2023

Rais mstaafu wa awamu ya nne na mkuu wa chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM) Dkt Jakaya Mrisho Kikwete,amefanya ziara katika mkoa wa Lindi kwa kutembelea katika maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la Tendegulu,sehemu ambayo aligundulika dinasoria,mnyama ambae aliishi miaka milioni 190 iliyopita na kutoweka miaka milioni 65 iliyopita.Mnyama huyo aliyegundulika na wajerumani baada ya kufanya utafiti wao mnamo mwaka 1908.

Lengo la ziara hiyo ni kutaka kufahamu kwamba mnyama huyo aliyegundulika huko tendegulu kama alikuwa mwenyewe au alikuwa na wenzake.Lakini pia kuanzisha mradi mkubwa wa utafiti kwa kuomba dunia iweze kutusaidia ili tuweze kufanikisha utafiti huo.

Vile vile ziara hiyo inakwenda sambamba na kutii agizo la serikali la kujenga chuo kikuu cha kilimo,chuo ambacho kitakua ni tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam(UDSM).

Sambamba na hilo moja ya mtafiti aliyekuja katika maeneo hayo ya tendegulu kutoka katika chuo kikuu cha Dar es salaam Dkt Pastory Bushozi katika maelezo yake mbele  ya wadau  waliohudhulia katika ziara hiyo alisema tafiti zinaonyesha kwamba  bahari ambayo inapatikana Lindi ilikuwa inaishia katika maeneo hayo ya Tendegulu na Dainosaria hao walikuwa wanatumia bahari hiyo kuja kunywa maji.Lakini pia alisema Dainosaria hao ambao walikuwa wanapatakina katika maeneo hayo ya Tendegulu walikuwa na mahusiano makubwa na Dinosaria ambao walipatikana South Afrika pamoja na Argentina.

Katika hatua nyingine Mhe.Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alipata wasaha wa kuona ramani ya chuo cha kilimo ambacho kinatarajiwa kujengwa katika eneo la Ngongo Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Pamoja na wilaya ya Ruangwa ambapo wanatarajia kufungua vyuo vya kilimo kwa shahada ya kwanza ,ya pili na ya tatu.Vyuo ambavyo vivitakwenda kufungua fursa mbalimbali ndani ya Mkoa wa Lindi na vitakuwa ni tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM).

Chuo ambacho kinakwenda kuanza ujenzi wake mwezi wa sita mwaka huu na inatarajiwa kuanza udahili wake wa kwanza mwaka 2025,miongoni mwa mambo ambayo yamepelekea chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM)  kufika Lindi kufungua tawi lake ni pamoja na kupanua ufundishaji katika digrii za awali na digrii za juu,lakini pia ni kuongeza uwekezaji ndani ya mkoa wa Lindi,kuongeza idadi ya watu ndani ya mkoa wa Lindi kutoka sehemu mbalimbali ambapo itapelekea mzunguko mkubwa wa fedha,vile vile Lindi ina sehemu nzuri za kilimo ambazo huwezi kuzipata katika maeneo mengine hapa nchini hivyo imepelekea chuo kikuu cha Dar es salaam kuvutiwa kufika mkoani Lindi na kufungua tawi lake.

Pamoja na hayo mke wa Rais mstaafu wa awamu ya nne na Mbunge wa jimbo la Mchinga Mama Salma Kikwete alitoa neno la shukrani kwa uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kwa ujenzi wa chuo cha kilimo ambacho kitakua ni tawi la chuo kikuu cha Dar es salaam,pia mama Salma alitoa wito kwa uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam kwa kuomba wakazi wa mkoa wa Lindi wapewe kipaumbele katika udahili wa masomo pindi kitakapo funguliwa, kwakua Lindi kuna wanafunzi  wengi ambao watahitaji kujiunga na chuo hicho.

Mwisho Mhe Rais mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete alisema Ngongo wamepewa hekta 45.2 kwaajili ya ujenzi ya chuo ambapo pia wanatamani waongezewe eneo lingine ili waweze kutanua chuo hicho kwasababu chuo kinahitaji eneo kubwa kwakua pesa za ujenzi wa chuo hicho zipo.Lakini pia wanahitaji kujenga ndaki nyingine ya chuo kikuu cha Dar es salaam maeneo ya Kagera,ambapo wameshapata maeneo ya kujenga tayari lakini pia wanahitaji kutanua chuo cha sayansi ya bahari huko Zanzibar ambapo pia pesa za ujenzi  zipo tayari.Vile vile alitoa wito kwa wakazi wa mikoa ya Lindi,Mtwara na Ruvuma kuanza  kujihusisha na kilimo cha soya kwasababu ni kilimo kizuri na kina mapato ya papo kwa papo ambapo tuta ongeza kipato cha mtu mmoja mmoja lakini pia kupelekea maendeleo katika taifa letu.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa