• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

UFUGAJI WA JONGOO BAHARI UPELEKEE KUONGEZA PATO LA HALMASHAURI-SILINDE

Imetumwa: March 31st, 2023


Naibu waziri wa mifugo na uvuvi Mhe. David Ernest Silinde (Mb) amefunga mafunzo ya ufugaji wa jongoo bahari ambayo yalikuwa yanafanyika katika Manispaa ya Lindi ukumbi wa chuo kikuu huria  kwa muda wa siku kwa muda wa siku 11 kuanzia tarehe 21 mpaka tarehe 30 mwezi huu.


Magunzo hayo yalikuwa yana husisha halmashauri tatu katika mkoa wa Lindi ikiwemo Halmashauri ya Mtama,kilwa na Manispaa ya Lindi.

Kwenye maelezo yake Mhe. Silinde alimpongeza Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazo zifanya katika kuleta maendeleo ya wa Tanzania kwa kuimarisha maisha ya wa Tanzania na kuyaboresha hususani ni wanawake.Lakini pia Mh.Silinde aliwapongeza washiriki wa mafunzo hayo wapatao 68 kwa kushiriki katika mafunzo hayo muhimu ya ufugaji wa jongoo bahari ambayo yanakwenda kufungua fursa za kiuchumi kwa mtu mmoja mmoja katika taifa letu.

Vile vile Mhe.Silinde aliwasihi washiriki wa mafunzo hayo kuendelea kutumia ujuzi ambao wameupata kwenye mafunzo hayo katika kujipatia maendeleo yao binafsi pamoja na taifa kwa ujumla.

Katika hatua nyingine Mhe.Silinde alielezea faida za ufugaji wa jongoo bahari katika kukuza kipato,upatikanaji wa chakula ,pamoja na ajira.Lakini pia jongoo bahari ni muhimu sana kwasababu hutumika katika kutengeneza lishe lakini pia katika kutengenezea dawa na vipodozi.

Ikumbukwe kuwa soko kuu la jongoo bahari ni china,thailand,korea kusini na marekani,ambapo kilo moja ya jongoo bahari wa daraja (A)ni Tsh 180,000 kwa kilo moja.Vile vile ufugaji wa jongoo bahari ni muhimu kwa utunzaji wa mazingira kwasababu jongoo bahari anasofa ya kusafisha bahari na kupunguza uchafuzi wa mazingira.

Katika hatua nyingine alisisitiza halmashauri zote ambazo zipo katika ukanda wa pwani kutoa vipaumbele kwa vijana wote ambao wamepata mafunzo ya FETA kuwapatia mikopo ili waweze kuanzisha vizimba vya ufugaji jongoo bahari 

Mwisho Mhe.Silinde alisisitiza washiriki kutumia wadau wa FETA katika kupata ujuzi na ushauri wa kitaalamu kuhusiana na kujihusisha na mazao ya bahari ikiwemo ufugaji wa jongoo bahari,mwani,kambakochi pamoja na kaa. Sambamba na hilo Mhe.Silinde alitoa vyeti kwa washiriki wote 68 kwa kushiriki katika mafunzo hayo muhimu kwa maendeleo ya taifa letu.




Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa