• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

TUZO NI MOTISHA NA KICHOCHEO KATIKA KUCHAGIZA UFANISI NA UTENDAJI KAZI KWENYE KUTOA MATOKEO CHANYA(RC-TELACK).

Imetumwa: April 9th, 2023

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe.Zainab Telack amewapongeza na kuwashukuru wadau mbalimbali wa elimu wakiwemo waalimu, wanafunzi pamoja na wazazi katika kuhakikisha watoto wanahudhuria  darasani na kupata elimu.

Pongezi hizo alizitoa siku ya jumamosi Aprili, 8 katika viwanja vya ilulu, Manispaa ya Lindi kwenye sherehe za uzinduzi wa mpango mkakati wa elimu mkoa wa Lindi kwa mwaka 2023, lakini pia utoaji tuzo kwa walimu,wanafunzi ,shule , kata na Halmashauri  pamoja na wadau mbao wamewezesha mkoa wetu kufanya vizuri kwenye mitihani wa upimaji ya kitaifa kwa mwaka2022.

Sambamba na hilo alipongeza walimu ambao waliandaa mabanda ya maonyesho kwaaijili ya mgeni rasmi na wageni waalikwa , lakini pia alipongeza waalimu wote wa shule za msingi na sekondari mkoa wa Lindi kwa kuongeza ufaulu katika shule zao na kupunguza idadi ya daraja la sifuri

Katika hatua nyingine mgeni rasmi alisisitiza waalimu kutoonyesha mitihani lakini pia waalimu wasimamie ufundishaji na ujifunzaji darasani kwa wanafunzi ili  kuwajenga wanafunzi waweze kuwa bora katika elimu zao.

vilevile mgeni rasmi alisisitiza ufanywaji wa mitihani ya ndani inayo ratibiwa na wilaya na mkoa ifanyike kwa wakati bila kuhairishwa wala kucheleshwa lakini pia  usahihisaji ufanyike kwa muda uliopangwa ili tuweze kupata matokeo na kufanya tathmini kwa maswali ambayo wanafunzi wameyakosea.Lakini pia mgeni rasmi alisisitiza walimu kuangalia nazaria mbalimbali za ufundishaji na kuwasaidia wanafunzi wote katika yale masomo ambayo yanawasumbua., kwa kuunda vikundi vya kujifunza ili waweze kujua masomo ambayo yanawasumbua.

Lakini pia Mhe. Mkuu wa mkoa bi Zainab Telack aliendelea kwa kusisitiza mambo mbalimbali kwa wageni waalikwa ikiwemo utoaji wa chakula mashuleni ili kuongeza umakini kwa mwanafunzi katika kupata maalifa, kupitia suala hili alitoa wito kwa waalimu kutoa elimu kwa wazazi kuhusiana na suala la utoaji wa chakula mashuleni,vilevile alitoa agizo kwa waalimu wa shule zote kuhakikisha wanaanzisha mashamba katika shule zao ili wanafunzi waweze kuzalisha chakula katika shule zao. Jambo lingine ambalo mkuu wa mkoa wa Lindi  Bi Zainab Telack alisisitiza lilikuwa ni kufanya ufuatiliaji na ufundishaji mashuleni , lakini pia alisisitiza kuimarisha mawasiliano ya mara kwa mara baina ya walimu,viongozi wa dini, na wazazi.Pia alisisitiza suala la kusimamia nidhamu ya wanafunzi wakiwa mashuleni.vilevile alisisitiza suala la kufanya  msawazo kwa walimu.Hatimae mkuu wa mkoa wa Lindi alitoa agizo kwa wakurugenzi na wakuu wa wilaya kwenye Halmashauri zote kuhakikisha walimu wanapata huduma za haraka pindi wanapofika ofisi za Halmashauri  ili waweze kupata muda wa kurudi shuleni na kama ikitokea changamoto yoyote basi mwalimu apangiwe tarehe ya kurudi tena na kupata ufumbuzi wa changamoto yake.Suala la usimamizi wa miradi ya ujenzi pia alizungumzia kwa kuhakikisha , miradi hiyo inaweza kukamilika kwa wakati kwani Rais wetu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania anafanya juhudi kubwa sana kaika kuhakikisha miradi hii inakamilika kwa wakati kwa kutoa fedha za ujenzi wa miradi hii, miradi hiyo ni kama vile miradi ya elimu,afya,maji na barabara.

  Mwisho mgeni rasmi katika sherehe hiyo Mhe, mkuu wa mkoa wa Lindi Bi Zainabu Telack alitoa zawadi kwa washindi mbalimbali kutoka katika wilaya zote za Mkoa wa Lindi.Sambamba na utoaji wa tuzo alizindua mpango  mkakati wa elimu mkoa wa Lindi kwa mwaka 2023.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa