• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

TAARIFA YA UFUNGAJI HESABU ZA HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI KWA MWAKA WA FEDHA ULIOISHIA 30 JUNI, 2021.

Imetumwa: September 29th, 2021

Taarifa za hesabu za mwisho za Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwa mwaka wa fedha 2020/2021 zimeandaliwa kwa mujibu wa Kanuni za uendeshaji wa Halmashauri kabla ya Hesabu hizi kuwasilishwa kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za Serikali (CAG) na zimeshawasilishwa na kujadiliwa  kwenye Kamati ya Timu ya Wataalamu (CMT),kikao cha Kamati ya ukaguzi (AC), Kikao cha Kamati ya Fedha na Mipango   na sasa  kwenye kikao cha Baraza Maalumu kwa ajili ya kupata idhini baada ya kujiridhisha na taarifa mbalimbali zilizomo katika Hesabu hizi.

Taarifa za hesabu za mwisho wa mwaka  za Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kwa mwaka wa fedha ulioshia tarehe 30 Juni 2021 pia  zinajumuisha   hesabu za Kata,Mitaa,Vijiji,Zahanati,Vituo vya Afya,Shule za Msingi na Sekondari na zimeandaliwa na kuwasilishwa kwa kuzingatia matakwa ya Viwango vya Kimataifa vya Uhasibu  katika Sekta ya Umma (IPSAS Accrual basis of Accounting).

 Taarifa kuu nne zinazojumuishwa kwenye taarifa za hesabu za mwisho wa mwaka  ambazo kisheria na kikanuni zinatakiwa ziidhinishwe kabla ya kukaguliwa na CAG  ni hizi zifuatazo:-

  • Mizania (Statement of Financial Position).
  • Taarifa ya mapato na matumizi (Statement of Financial Performance).
  • Taarifa ya mtiririko wa fedha Taslimu (Cash Flow Statement).
  • Taarifa ya Mabadiliko ya Mtaji (Statement of Changes in Net Asset)

MIZANIA (Statement of Financial Position)

Mizania ni taarifa inayoonesha mali zinazomilikiwa na Halmashauri pamoja na madeni inayodaiwa hadi kufikia tarehe 30 Juni 2021, taarifa hii inaonesha kuwa Halmashauri hadi kufikia tarehe 30 Juni 2021 ilikuwa na mali zenye thamani ya TZS. Bilioni 42.240 ambapo mali za kudumu ni TZS. Bilioni TZS. 40.878 na za muda mfupi   ni TZS. Bilioni 1.363.

Vilevile Mizania inaonesha kuwepo kwa madeni yenye jumla ya TZS. Billioni 3.781 ambapo madeni ya muda mrefu ni TZS. Milioni 5.242   na madeni ya muda mfupi ni TZS. Bilioni 3.776

TAARIFA YA MAPATO NA MATUMIZI (Statement of Financial Performance).

  • Taarifa hii inaonyesha jumla ya mapato na matumizi yote ya Halmashauri kwa mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2021 ambapo Halmashauri ilipokea na kukusanya jumla ya TZS.Bilioni 16.087 kutoka katika vyanzo mbalimbali, mapato yameongezeka kwa TZS. Bilioni 2.054 ukilinganisha na mwaka wa fedha ulioishia 30 Juni 2020 ambapo mapato ya Halmashauri yalikua ni TZS. Bilioni 14.032.
  • Kwa upande wa matumizi Halmashauri ilitumia jumla ya TZS. Bilioni 14.432 hadi kufikia tarehe 30 Juni 2021 ambapo matumizi yameongezeka kwa TZS. Milioni 460.223 ukilinganisha na mwaka wa fedha ulioishia tarehe 30 Juni 2020 ambapo matumizi ya Halmashauri yalikua TZS Bilioni 13.971.

TAARIFA YA MTIRIRIKO WA FEDHA TASLIMU (Cash Flow Statement)

Taarifa hii huonyesha mwenendo wa mapokezi ya fedha taslimu kwa mwaka mzima kutoka katika vyanzo mbalimbali vya Halmashauri (OSR) pamoja na ruzuku kutoka serikali kuu na matumizi yake kwa mwaka wa fedha husika. Kwa mwaka wa Fedha unaoishia 30 Juni 2021 Halmashauri ilipokea na kukusanya pesa taslimu kiasi cha TZS. Bilioni 14.374 kutoka vyanzo vya ndani pamoja na ruzuku na kutumia kiasi cha TZS. Bilioni 12.620 kwenye matumizi mishahara na shughuli za kawaida,kiasi cha fedha TZS. Bilioni 3.024 zilitumika katika shughuli za uwekezaji na kiasi cha TZS. 75.662 Kilitumika katika shughuli za kifedha (Mikopo ya Wanawake Vijana na Watu wenye Ulemavu). Hadi kufikia tarehe 30 Juni Mwishoni Halmashauri ilibakiwa na jumla ya fedha taslimu TZS. Milioni 247.994 kwenye akaunti mbalimbali (Kata,Vijiji,Mitaa,Shule za Sekondari na Msingi,Zahanati Vituo vya Afya na Ofisi kuu)

Taarifa ya Mabadiliko ya Mtaji (Statement of Changes in Net Asset)

Taarifa hii inaonesha mabadiliko ya mtaji ambapo mabadiliko haya yanatokana na ziada au pungufu ya taarifa ya mapato na matumizi (Surplus/Deficit) kwa mwaka wa fedha husika. Kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni 2021, Mtaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ulibadilika kutokana na miamala ifuatayo:

  • Ziada ya inayotoka kwenye taarifa ya mapato na matumizi ya mwaka unaoishia 30 Juni 2021 Kiasi cha TZS. Bilioni 1.655 ambayo ilipelekea kuongeza mtaji wa Halmashauri (Net Assets).
  •  Kuongezwa kwa Jimbo la Mchinga kwenye Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kumepelekea mtaji kuongezeka. Hii inatokana na mali za kudumu zenye thamani ya kiasi cha TZS. Bilioni 7.032, Ardhi TZS. Milioni 57.8 pamoja madeni ya vikundi vya Wanawake, Vijana na Watu wenye Ulemavu kiasi cha TZS. Milioni 12.558.
  • Fedha zilizobaki kwenye Akaunti ya Wanawake Vijana na Watu wenye ulemavu kiasi cha TZS. Milioni 28.771 ambazo hazikujuishwa kwenye hesabu za mwaka wa fedha ulioshia 30 Juni 2020.
  • Malipo ya awali kiasi cha TZS. Milioni 751.563 ambayo hayakujumuishwa kwenye hesabu za mwaka mwaka wa Fedha ulioshia 30 Juni 2020
  • Miamala yote hii imepekelea mtaji wa Halmashauri kufikia kiasi cha TZS. Bilioni 38.429 kwa mwaka wa fedha unaoishia 30 Juni 2021

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa