• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

SIKU YA WANAWAKE DUNIANI NI SIKU YA KUJIKUMBUSHA WAJIBU PAMOJA NA MAJUKUMU YETU . RC-TELACK

Imetumwa: March 8th, 2023

Tarehe 8 Machi kila mwaka tuna sherehekea siku ya wanawake duniani ambapo kwa mkoa wa Lindi kama ilivyokuwa kwa mikoa mingine pia tulitumia siku hii katika kujikumbusha harakati pamoja na juhudi  zinazofanywa na mwanamke katika kuleta maendeleo ya jamii na taifa kwa ujumla.

Katika maadhimisho ya siku ya wanawake kwa mkoa wa Lindi mwaka huu, 2023 yalipata kufanyika kaika wilaya ya Nachimgwea na mgeni rasmi katika maadhimisho hayo alikuwa ni Mhe. Zainab Telack,mkuu wa mkoa wa Lindi.

Mengi yalizungumzwa katika maadhimisho hayo ikiwemo mambo mbalimbali ya kimaendeleo kuhusiana na wanawake,lakini pia kwenye maadhimisho hayo burudani pia kutoka katika vikundi mbalimbali zilikuwepo.Ikiwemo taasisi pamoja na idara mbalimbali kama vile jeshi la polisi,TANESCO,Afya,kilimo.

Awali akiongea na wananchi wa Nachingwea mbunge wa jimbo la Nachingwea Dkt. Amandus Chinguile alisema mpongeza  Dkt Samia Suluhu Hassan kwa maendeleo anayo yafanya kwaajili ya nchi yetu,lakini pia alitumia nafasi hiyo kumpongeza mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack kwa jitihada zake kubwa anazo zifanya kwaajili ya maendeleo ya mkoa wetu.


Katika hatua nyingine mbunge wa viti maalum mkoa wa Lindi Mhe Tecla Ungele,alipata nafasi ya kuongea na wanawake wa Nachingwea  kwa kumuombea kura Mhe. Dkt Samia Suluhu Hassani kwaajili ya uchaguzi ujao wa mwaka 2025.lakini pia alizungumzia suala la ukatili wa kijinsia kwa wanawake na kukemea kitendo hicho.

Sambamba na hilo mbunge wa jimbo la Mchinga Mhe Salma Kikwete, alipata nafasi ya kuongea na wanawake waliohudhuria katika maadhimisho hayo ya siku ya wanawake duniani,kwa kumpongeza Rais wa jamhuri waJmhuri ya muungano wa Tanzania Dkt .Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa anazo zionyesha katika kuleta maendeleo ya nchi yetu,katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu ,afyapamoja na miundombinu


Kwenye maadhimisho hayo pia shughuli mbalimbali za kijasiliamali ambazo zinafanywa na wanawake zilikuwepo,wanawake walipata kuonyesha shughuli zao mbalimbali kwenye mabanda yao.Wanawake wa Manispaa ya Lindi pia walikuwa na banda lao  katika maonyesho hayo,banda ambalo lilikuwa limesheheni bidhaa mbalimbali za kijasiliamali kama vile batiki,mikoba,vitafunwa pamoja na pilipili.Banda hilo la wanawake wa Manispaa ya Lindi ni miongoni mwa banda ambalo lilipata kutembelewa na mgeni rasmi Mhe Zainab Telack.

Wakisoma risala yao wanawake wa mkoa wa Lindi walielezea jinsi mkoa wa Lindi ulivyo shikwa hatamu na wanawake akiwemo mkuu wa mkoa pamoja na wabunge.kwenye risala hiyo pia wanawake walishukuru kwa kuwezeshwa kupata elimu za uzalishaji, ujasiliamali pamoja na biashara kupitia idara ya maendeleo ya jamii pamoja na vikoba.Wanawake pia wameweza kutatua migogogro ya kifamilia.Pia alielezea changamoto ambazo wanawake wanakumbana nazo kama wanawake ikiwemo baadhi ya wanaume kutotambua usawa wa kijinsia hivyo kupeleka ugumu katika kuleta maendeleo,vilevile kunyanyapaliwa kwenye baadhi ya shughuli ikiwemo udereva.  

Mwisho, mkuu wa Mkoa wa Lindi Mhe. Zainab Telack alipata nafasi ya kuhutubia wananchi ambao walihudhuria katika maadhimisho hayo ya siku ya wanawake kwa kuwasisitiza wanawake kuwa siku hiyo ni siku ya kujikumbusha,majukumu na wajibu wa mwanamke,Telack pia aliwaomba wanawake kujiunga katika vikundi ili waweze kufanya shughuli mbalimbali za biashara na ujasiliamali kutokana na kuwepo kwa fedha katika halmashauri kwaajili ya maendeleo ya wanawake na walemavu.Telack pia aliwaomba wazazi wasomeshe watoto wao kwaajili ya maendeleo ya nchi yetu,kwasababu Dkt. Samia Suluhu Hassan ametoa fedha kwaajili ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari ili watoto wapate elimu bora.Telack pia aliwaomba wanawake waweze kuwatunza wanaume  pamoja na watoto wao.Pia aliwaomba waalimu kuwaangalia wanafunzi wakati wakiwa mashuleni,Hatimae , Mhe.Telack aliwaomba wananchi pamoja na viongozi wa dini kufanya maombi ya kuomba mvua kulingana na kuongezeka kwa jua mkoani kwetu


Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa