• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

SHULE YA SEKONDARI MILOLA NA SHULE YA MSINGI NGWENYA KUNUFAIKA NA MRADI WA TPP

Imetumwa: February 8th, 2023

Ziara ya wageni kutoka katika chuo kikuu cha Michigan,chuo kikuu cha Dar es salaam (UDSM),chuo kikuu cha sokoine cha kilimo(SUA),pamoja na Chuo kikuu kishiriki cha elimu Dar es salaam (DUCE) imefanikiwa kwa kuweza kufungua miradi yote ambayo imenzishwa katika kijiji cha Milola. Kwa sasa mradi huu wa TPP unatekelezwa sehemu mbili Hapa Tanzania ambazo ni Monduli katika kijiji cha Naitolia pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Lindi katika kijiji cha Milola.

Miradi hiyo ni pamoja na ufunguzi wa bweni moja la wasichana pamoja na darasa moja la awali ambapo bweni hilo linachukua wanafunzi 104 lakini hata hivyo maombi ya wanafunzi kuishi kwenye bweni ni mpaka sasa ni makubwa.Hiyo ni kutokana na kuongezeka kwa ufaulu katika shule hiyo hususani kwa upande wa wasichana, hiyo ni kutonana na kupatikana kwa ufaulu wa daraja la kwanza (division one)kwa msichana kitu ambacho kilikuwa hakijawai kutokea katika historia ya shule hiyo.Kupitia bweni hilo katika shule ya sekondari Milola inapelekea kupunguza idadi kubwa ya wasichana ambao wamekuwa wakitembea umbali mrefu kwaajili ya kupata elimu kwenye kijiji hicho cha Milola.

Mradi mwingine ambao umepata kufunguliwa ni darasa moja kwa elimu ya awali katika shule ya msingi Ngwenya,ufunguzi wa darasa hilo la awali inapelekea watoto kupata elimu ya awali na kuounguza umbali mrefu wa kutembea kwa watoto hao

Kwenye hotuba yake kabla ya ufunguzi wa beeni hilo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi Ndg, Juma Mnwele amewaomba wazazi katika kijiji hicho cha Milola kuchangia chakula kwaajili ya wanafunzi ambao wanaishi kwenye bweni hilo.Lakini pia alisema Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ina mpango wa kupandisha hadhi shule hiyo ya sekondari Milola kwa kuongeza kidato cha tano na kidato cha sita.

Sambamba na hilo Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Milola  amesema shule ya sekondari Milola ni shule ya kata ambayo inachukua kitoka katika maeneo mbalimbalii ya Milola ikiwemo Kiwawa,Mputwa,Legeza mwendo,Milola B,Milola Mashariki na Milola magharibi.Lakini pia aliongozea kwa kusema baadhi ya wanafunzi wanatoka mbali na shule hiyo umbali wa kilometa 20 mpaka kufika shuleni hapo kwa kutumia usafiri wa baiskeli.

Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya sekondari Milola  amesema ufaulu wa shule hiyo kwa kipindi cha nyuma ulikuwa sio mzuri kwa jinsia zote wavulana na wasichana.Lakini baada ya ujenzi wa bweni hilo ufaulu umeongezeka hususani kwa upande wa wasichana.Lakini pia kwenye hotuba yake mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Milola alisema TPP imetoa mwalimu mmoja wa somo la Historia,uraia pamoja na fasihi ya somo la kingereza.Lakini pia TPP inatoa waalimu ambao wapo masomoni kutoka katika chuo kikuu   kishiriki cha elimu (DUCE),kila mwaka.Lakini pia kama shule imetoa mwalimu mmoja kwaajili ya kufundisha somo la Jiografia pamoja na kingereza hii yote ni kuthamini jitihada zinazo tolewa na TPP.

Lakini pia mwalimu mkuu alitoa shukrani kwa niaba ya uongozi wa shule ya sekondari Milola,kwa kuwashukuru TPP kutokana na mchango wao mkubwa wanao utoa katika shule hiyo ya sekondari Milola,kwenye upande wa taaluma kwa kusaidia kupandisha ufaulu wa shule hiyo kwa wanafunzi lakini pia kupunguza umbali kwa wanafunzi wa shule hiyo kufuata elimu kutoka vijiji vya mbali.

Mwisho timu ya TPP ikishirikiana na uongozi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi ilitoa zawadi kwa mwanafunzi aliyefanya vizuri katika masomo yake ya kuhitimi kidato cha nne katika shule hiyo ya sekondari Milola,Salama Omari Makalani, kwa kupata ufaulu wa daraja la kwanza katika masomo yake ya kuhitimu kidato cha nne kwa kupata daraja la kwanza la kwa pointi 15. Ambapo inahusisha (A) 2 (B) 2 pamoja na (C) 6.Katika  matokeo hayo amepata (A) ya somo la hisabati pamoja (A) ya somo la Kemia.Matokeo ya mwanafunzi huyo ni matokeo ya mradi wa TPP,kwani hayakuwai kutokea kwa upande wa wasichana  tangu kuanzishwa kwa shule

Katika hatua nyingine salama alishukuru wazazi kwa malezi mazuri waliyompatia lakini pia  aliwashukuru TPP kwa kujenga bweni katik shule hiyo kwani wamekuja kubadilisha maisha ya wanafunzi katika shule hiyo kwa kuongeza ufaulu katika shule hiyo,vilevile aliwashukuru walimu kwa juhudi kubwa wanazofanya kwa wanafunzi wa shule hiyo ili kuongeza ufaulu,Salama pia aliwasihi wanafunzi wenzie kusoma kwa bidii iliwaweze kupata matokeo mazuri kama yeye au zaidi yake.

Mwisho timu ya TPP pamoja na mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi walipata nafasi ya kufungua bweni hilo la wasichana katika shule ya sekondari Milola.Baada ya ufunguzi wa bweni katika shule ya sekondari Milola,msafara uliekea katika shule ya Msingi Ngwenya ambapo pia ulifanyika ufunguzi wa darasa moja la awali katika shule hiyo ya msingi Ngwenya.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • MJUMBE WA TUME HURU YA TAIFA YA UCHAGUZI ATEMBELEA VITUO VYA UANDIKISHAJI HALMASHAURI YA MANISPAA YA LINDI.

    May 17, 2025
  • ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA AWAMU YA PILI MANISPAA YA LINDI LIMEANZA LEO MEI 16,2025.

    May 16, 2025
  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa