• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MHE. NDEMANGA AFUNGUA MADARASA SHULE YA SEKONDARI MILOLA

Imetumwa: December 21st, 2022

Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe. Shaibu Ndemanga,amefanya ufunguzi wa madarasa matatu ya kidato cha kwanza yatakayo anza kutumika mapema mwakani 2023.

Mradi huo wa madarasa matatu ambayo una thamani ya Shilingi milioni 60, ni moja ya jitihada zinazofanywa na rais wetu Dkt Samia Suluhu Hassan kuhakikisha Watoto wanapata elimu bora. Akielezea taarifa fupi ya shule ya sekondari Milola, mkuu wa shule hiyo alisema shule ya sekondari Milola ilianzishwa mwaka 2004 ikiwa na idadi ndogo ya wanafunzi na miundombinu yake. Kwasas shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 378 kati ya hao Wavulana ni 167 na wasichana ni 211 lakini kwa mwaka 2023 shule hiyo inatarajia kuwa na wanafunzi 598 ambapo Wavulana ni 258 na Wasichana ni 340, aidha mwalimu mkuu alisema shule hiyo ina jumla ya walimu 10  na mmoja wa kujitolea kwa ufadhili wa Tanzania Partnership Program (TPP),kati ya walimu hao Wanaume ni 8 na wanawake 2 pamoja na huyo anayejitolea kwa ufadhili nae ni Mwanaume. Aidha mwalimu mkuu wa shule hiyo  amesema shule ya sekondari Milola ina jumla ya vyumba 14 vya madarasa Pamoja na hivyo vipya, ofisi mbili  za walimu na maabara 3,pia ina vyoo 10 vya wanafunzi Wavulana vyoo 5 na Wasichana 5.

Mwalimu mkuu alisema mnamo tarehe 1/10/2022 walipokea kiasi cha fedha cha ujenzi wa madarasa matau kiasi cha shilingi milioni 60 kupitia akaunti ya shule. Baada ya hapo  walianza kuhitisha vikao vya kutambulisha mradi ngazi ya kata na uteuzi wa fundi.

Aidha mwalimu mkuu alisema ujenzi rasmi wa shule hiyo  ulianza rasmi tarehe 28/ 10/2022 kwa kasi kubwa.Vile vile  mkuu wa shule a;lisema usimamizi wa ujenzi huo ulisimamiwa na walimu wote licha ya kuwa na kamati tatu kama vile kamati ya Ujenzi, kamati ya Manunuzi na kamati ya Mapokezi.Pia walikua Pamoja wakati wote na wajumbe wa bodi ya shule na viongozi wa ngazi ya kata.Hata hivyo viongozi wa ngazi ya Manispaa pia walihakikisha mradi huo una kamiloika vizuri.

Mkuu wa shule alisema ujenzi huo wa madarasa matatu umekamilika tangia 2/12/2022.Mfumo wa umeme, viti 150 na meza 150 pamoja na sakafu iliyo wekwa  malumalu.Mwalimu mkuu alisema vipo vifaa vya ujenzi ambavyo vimebakia ambavyo ni Saruji mifuko 46, bati 1, tofali 400 pamoja na malumalu boksi 4. Ambapo mwalimu mkuu alitumia nafasi hiyo kumuomba mkuu wa wilaya kuruhusu vifaa hivyo vilivyo bakia kutumika katika kukarabati ofisi na madarasa lakini pia  baadhi ya sehemu katika majengo hayo ya shule ikiwemo ofisi ya waalimu Pamoja na vyoo.

Pia mkuu wa shule alielezea changamoto ambazo walikutana nazo wakati wa kipindi cha ujenzi wa madarasa hayo,ikiwemo uhaba wa maji,lakini pia pamoja na elimu kwa jamii kuhusiana na suala la  kujitolea.

Katika hatua nyingine mkurugenzi wa Halmashuri ya Manispaa ya lindi Ndg, Juma Mnwele aliongezea kwa kutaja maeneo mengine ndani ya Manispaa ya Lindi ambayo yanaendelea na mradi huu ujenzi wa madarasa Kumi yenye thamani ya shilingi milioni 400,ambayo ilipatikana tarehe 1/10 mwaka huu,pia alitaja maeneo mengine ambayo mradi huo unatekelezwa ambayo ni Shule ya sekondari Kitomanga darasa 1 ,Shule ya sekondari Mipingo darasa 1 ,Shule ya sekondari Mvuleni, darasa 1,Shule ya  sekondari Angaza Lindi mjini madarasa 2,Shule ya sekondari Mingoyo madarasa 4 , Madarasa 2 shule ya sekondari Ng’apa lakini pia  madarasa 3 shule ya sekondari Milola, lakini pia madarasa 3 shule ya sekondari Nangalu, Pamoja na madarasa 3 Shule ya sekondari Milola.

Sambamba na hilo Mkuu wa wilaya ya Lindi Mhe.Shaibu Ndemanga alipata nafasi ya kuzungumza na wananchi waliohudhuria katika kikao hicho cha ufunguzi wa madarasa 3 katika shule hiyo,Ndemanga alichukua nafasi hiyo kumshukuru Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutupatia kiasi cha fedha cha shilingi milioni 400 kwaajili ya ujenzi wa madarasa katika Manispaa ya Lindi.

Lakini pia Ndemanga aliwaomba viongozi wa Kijiji hicho cha Milola kuhakikisha wanafuatilia kwa kalibu wanafunzi ambao wamechaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2023,kuhakikisha wanafika mashuleni na kuanza masomo yao ifikapo Januari 9.Kwa kufanya hivyo itasaidia kukamilisha mradi huo, kwasababu lengo la kufanya ujenzi wa madarasa hayo ni kuhakikisha wanafunzi wanapata elimu bora.

Mwisho mgeni rasmi na wageni waalikwa walienda kutembelea moja ya mradiambao unafanyika katika shule hiyo ambao ni mradi wa  wa ufugaji wa kuku wa nyama na kuku wa mayai, mradi huo una simamiwa na Tanzania Partneship Program (TPP) ,mradi ambao wanafunzi wa shule hiyo  huwasaidia kupata ujuzi wa Maisha na kuwasaidia katika kujiari baada ya kuhitimu masomo yao ya sekondari.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa