• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MKOA WA LINDI UNA MAENEO YA KUTOSHA KWA SHUGHULI ZA KILIMO NA UFUGAJI-MABULA

Imetumwa: December 29th, 2022

Mkuu wa mkoa wa Lindi Mhe. Zainabu Telack akiongea na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Lindi kutoka katika Wilaya na Halmashauri zote.katika kikao hicho ambacho kilihudhuliwa pia na Waziri wa Nchi nyumba na maendeleo ya makazi Dkt Angelina Mabula ambae pia ni mwenyekiti wa timu hiyo ya utatuzi wa migogoro mbalimbali, akiwa sambamba na mawaziri wanane wakisekta kutoka katika sekta tofauti tofauti kama vile Waziri wa maliasili na utalii lakini pia aliongozana na manaibu Waziri wa kilimo,pia aliongozana na naibu Waziri wa mifugo na uvuvi,lakini pia naibu Waziri ofisi ya makamu wa Rais mazingira,pia aliongozana na naibu Waziri wa maji,  pia kikao hicho kilihudhuliwa na wataalamu wa mambo mbali mbali kama vile naibu katibu mkuu kutoka wizara ya  maji,kaimu katibu mkuu kutoka katika wizara ya mifugo na uvuvi lakini pia kaimu katibu mkuu maliasili,vile vile aliongozana na afisa Habari wa wizara ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi,Pamoja na makatibu Waziri watatu,Kikao ambao kilikuwa na lengo la kutatua migogoro baina ya vijiji na hifadhi za serikali ambapo ina husisha misitu ya TFS Pamoja na misitu mingine.

Katika maelezo yake Telack alisema ‘’Yapo maeneo ambayo wananchi wame ingia kwenye hifadhi lakini pia yapo maeneo  mengine  ambayo wananchi wameingia kwenye vyanzo vya maji kwa mfano Mtopera,mto ambao wananchi wamekwenda kufanya shughuli zao za uzalishaji pembezoni mwa mto. Mto ambao ni tegemeo kubwa kwa Wanyama pori ambao wanaishi kwenye hifadhi hiyo, kama mto huo utahifadhika itakua ni Faraja kubwa sana kwasababu unasaidia ikololijia lakini pia uweze kuungana na mito mingine,ili iweze kujaza bwawa la Mwl Nyerere”.

Katika hatua nyingine Telack pia aliwakumbusha wakulima waweze kulima katika maeneo yao, kwasababu Lindi kuna maeneo mengi na yakutosha.Hivyo hatuna sababu ya kugombana kwasababu yapo maeneo ya kutosha.Lakini pia alisema kwa kila Halmashauri wametenga maeneo kwaajili ya wafugaji,hivyo alisisitiza wafugaji kukaa kwenye maeneo yao ambayo yametengwa kwasababu yapo.

Lakini pia alitumia fursa hiyo kuzungumzia mambo mbalimbali ya uwekezaji yanayo patikana Lindi  ikiwemo suala la mradi mkubwa  wa gesi wa LNG,mradi ambao ni fursa `     kubwa kwa wakazi wa Lindi lakini pia kwa watu kutoka sehemu mbalimbali hivyo alisisitiza wageni kuja kuwekeza mkoani hapa.Vile vile alisema  Lindi kuna bahari nzuri ambayo inafaa kwa utalii na uwekezaji, pia Lindi kuna mradi wa ujenzi wa chuo kikuu cha kilimo ambacho kina simamiwa na chuo kikuu cha Dar es salaam.Pia alizungumzia ujenzi wa chuo kikubwa cha ufundi Afrika Mashariki,chuo ambacho kinaenda kuwekwa jiwe la msingi mwezi wa pili mwakani.

Vile vile Mkuu wa mkoa alitumia nafasi hiyo kuwakaribisha wageni hao ambao walihudhuria katika kikao hicho kuja Lindi kwasababu kuna vitu vingi vya kuvutia ambavyo vina weza kuwa vivutio vya utalii lakini pia kuongeza uchumi katika taifa letu, upatikanaji wa bahari ambayo ina beba aina tofauti za Samaki pia ni kitu cha pekee ambacho kina patikana lindi’.

Mwisho Waziri wa Nchi nyumba na maendeleo ya makazi nae alipata nafasi ya kuzungumza na wageni waalikwa kwa kusema’’ Mkoa wa Lindi una vijiji 11 ambavyo havipaswi kuingia kwenye msitu wa Nyengedi na hifadhi ya Selous kwaajili ya Kwenda kufanya shughuli mbalimbali za uzalishaji ikiwemo kilimo na ufugaji.Mabula alivitaja vijiji hivyo abavyo ni Mtakuja,Mkanga,Mtauna,Zinga kibaoni,Pamoja na Mtopera, nakubainisha kwamba wakazi wa maeneo hayo hawapaswi kuingia katika hifadhi kwasababu tayari wana maeneo yao ya kutosha ambayo yame wekwa maalumu kwa ajili ya shughuli za makazi na uzalishaji.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa