• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE MANISPAA YA LINDI YAFANA.

Imetumwa: March 6th, 2023

Maadhimisho ya siku ya wanawake Manispaa ya Lindi ambayo yamefanyika katika kata ya Ng'apa kiwanaja cha shule ya msingi Ng'apa yalifanyika tarehe 6 Machi mwaka huu ambapo wageni mbalimbali kutoka ndani ya Manispaa ya Lindi kama vile mstahiki meya wa manispaa ya Lindi Mhe, Frank Magali,madiwani wa kata mbalimbali zilizopo ndani ya Manispaa ya Lindi,mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mhe.Juma Mnwele wakuu mbalimbali wa idara,viongozi wa taasisi na asasi mbalimbali za kiraia,waalimu pamoja na wanafunzi walipata kuhudhuria maadhimisho hayo ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mbunge wa jimbo la Lindi Mjini Mhe Hamida Abdallah.

Kwenye maadhimisho hayo michezo mbalimbali ilifanyika ambapo washiriki wa michezo hiyo yote walikuwa ni wanawake,michezo hiyo ni kama vile kufua nazi,kukuna nazi,kuendesha baiskeli,kukimbia na magunia,pamoja na kucheza rede.Katika michezo hiyo yote ambayo wananwake wa kata ya Ng'apa walipata kushiriki,zawadi mbalimbali zilitolewa kwa washindi wote.


Sambamba na michezo hiyo iliyochezwa na wanawake, pia katika maadhimisho hayo vikundi mbalimbali vya burudani kutoka katika maeneo mbali vilipata kutoa burudani mbele ya mgeni rasmi pamoja na wageni waalikwa.Miongoni mwa burudani zilizo tolewa ni pamoja na ngoma,maigizo pamoja na ngonjera.

Akizumgumza na wageni waalikwa katika maadhimisho hayo mgeni rasmi Mhe. Hamida Abdallah(mbunge) alishukuru serikali ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuruhusu maadhimisho hayo ya siku ya wanawake kuendelea kufanyilka miaka yote,lakini pia aliwashukuru kamati ya maandalizi ya sherehe ya wanawake duniani  kwa kumuamini na kuwa mgeni rasmi.Lakini pia alimpongeza mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi kwa kuthamini kata zilizokuwa mbali na mjini kupeleka sherehe hiyo ya maadhimisho ya wanawake katika kata hiyo..

Katika hatua nyingine kwenye maadhimisho hayo, mengi yamezungumziwa kuhusiana na maendeleo ya mwanamke, lakini pia utekelezaji wa miradi mbalimbali ambayo imeanzishwa Kwenye kata ya Ng'apa Kupitia serikali ya jamhuri ya muungano wa Tanzania,chini ya Dkt Samia Suluhu Hassan.Miradi hiyo ni kama vile kituo kikubwa cha afya katika kata ya Ng'apa,ambacho kimeghalimu Kiasi cha fedha shilingi Milioni 500,ambapo kituo hicho kimekamilika na kinatoa huduma kwa wakazi wa kata ya Ng'apa.

Sambamba na hilo alielezea hatua zinazo endelea katika kituo cha afya Ng'apa kuwa ni ununuzi wa Mashuka,vitanda pamoja na mashine za BP ili kupunguza tatizo la kujifungua kwa wanawake wa kata hiyo ya Ng'apa.

Lakini pia Mhe.Mbunge amehakikisha wakazi wa kata ya  Ng'apa wanaendelea kupata huduma bora za afya kwa kuchangia kiasi cha fedha shilingi Milioni 4,750,000.Kwaajili ya ujenzi wa zahanati,aidha ametoa agizo kwa  mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi Mhe.Juma Mwele kuchangia ujenzi wa zahanati hiyo kiasi cha fedha shilingi Milioni 4,000,000 kutoka kwenye mfuko wa jimbo ili kuhakikisha wananchi wa Ng'apa wanaendelea kupata huduma bora za Afya.Lengo ni kuhakikisha wamama wajawazito wanapata huduma bora wakati wa kujifungua.

Mwisho Mhe,Hamida alifanya ufunguzi wa jukwaa la uwezezaji kiucumi la wanawake ambapo kata ya Ng'apa imekuwa ni kata ya kwanza katika kufungua jukwaa hilo la kiuchumi kwa wanawake.Mhe. Hamida alimkabidhi mstahiki meya wa Manisopaa ya Lindi vitanda 10 vya kujifungulia ,mashine kumi,pamoja na mashuka 50 kwaajili ya zahanati4 zilizo jengwa kupitia fedha zilizo tolewa na Dkt Samia Suluhu Hassan,Zahanati hizo ni zahanati ya Tandangongoro,mtanda,banduka pamoja na Ruaha.Lakini pia Mhe. Hamida alikabidhi viti 100 kwa shule ya sekondari Ndemanga.Vilevile alitoa  tofali 3000 kwaajili ya ujenzi wa zahanati, ambapo tofali 1000 zinakwenda kwenye ujenzi wa zahanati ya Ng'apa,tofali 1000 kwaajili ya ujenzi wa zahanati ya Mkwaya na tofali 1000 katika ujenzi wa zahanati ya Nachingwea ili kuongeza ukubwa wa chumba cha kujifungulia  katika zahanati hiyo."Kauli mbiu ya maadhimisho ya siku ya wanawake dunian kwa mwaka huu 2023 ni"Ubunifu na mabadiliko ya kiteknojia chachu katika kuleta usawa wakijinsia".



Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa