• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

KAMATI YA LAAC YAPONGEZA UONGOZI NA WALIMU WA SHULE YA SEKONDARI LINDI PAMOJA NA KUTOA MAELEKEZO KWA TAMISEMI

Imetumwa: March 23rd, 2023

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa(LAAC) imewapongeza viongozi na walimu wa Shule ya Sekondari Lindi kwa kuhakikisha wanatimiza wajibu wao kwenye usimamizi wa rasilimali fedha na watu na kuifanya elimu kuwa bora na kuongeza ufaulu Mkoani Lindi

Hayo yamesemwa Machi 23, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mhe. Halima Mdee (Mb) wakati wa ziara ya kikazi ya kukagua miradi ya maendeleo katika Manispaa ya Lindi Mkoani Lindi.

Lengo la ziara hiyo katika shule ya sekondari Lindi ni kutaka kujua matumizi ya fedha zilizotolewa na serikali zilivyotumika  kwa ajili ya ukarabati.

Mdee alisema “hii kamati ya LAAC inawakilisha Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni vizuri tujue fedha hizi zilizoletwa hapa zimetumikaje” .

Awali akisoma taarifa Mkuu wa Shule ya Sekondari Lindi Bw. Ramadhani Divele ameishukuru Serikali kwa kuendelea kuboresha na kuweka mazingira mazuri katika sekta ya elimu ambapo zaidi ya shilingi milioni 725 na zilitolewa kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo.

Amefafanua kuwa fedha hizo zilifanya ukarabati wa vyumba vya madarasa 17, nyumba za walimu 7, mabweni 6, bwalo la chakula 1, matundu ya vyoo 37 maabara 3 na kuweka mifumo ya gesi na maji, jengo la utawala, jiko na stoo ya chakula.

Lakini pia Amesema fedha hizo za ukarabati zilitokana na programu ya EP4R lakini pia shule ilipokea tsh. milioni 10 kutoka Ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Lindi kwa ajili ya kulipia gharama za maji na mafundi waliokuwa wamekarabati nyumba sita za walimu.

Katika hatua nyingine Divele alisema uwepo wa mazingira rafiki ya kujifunzia na kufundishia imesaidia kupanda kwa taaluma lakini pia umoja na ushirikiano baina ya walimu kwa walimu, wanafunzi kwa walimu na wanafunzi kwa wanafunzi amewezesha kufanya vizuri kwenye mitihani ya kidato cha sita kwa miaka mitatu kutoka 2020-2022.

Vilevile  Divele  alisema shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,448 wasichana 460 na wavulana 988 na kwa upande wa kidato cha nne inafanya vizuri na kuendelea na jitihada kuhakikisha ufaulu unaongezeka na kufika asilimia 100.

Sambamba na hilo Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeitaka Ofisi ya Rais –TAMISEMI kufanya uchunguzi na kuchukua hatua kwa watendaji watakaobainika wamekiuka Sheria, Kanuni na Taratibu za utekelezaji wa miradi ya mendeleo .

Hayo yamebainishwa leo tarehe 24 Machi, 2023 na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa Mhe. Halima Mdee (Mb) wakati wa majumuisho wa ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Nachingwea, Halmashauri ya Wilaya ya Mtama na Manispaa ya Lindi, Mkoani Lindi.

“hii sio tu kwa Halmashauri hizi za Mkoa wa Lindi hapa nazungumzia Halmashuri zote nchini watendaji wanaokiuka kufuata Taratibu, Sheria na Kanuni za utekelezaji wa miradi wachukulie hatua”amesisitiza Mhe.Mdee

Mdee ameishauri Ofisi ya Rais –TAMISEMI kushughulikia suala la ongezeko la watumishi katika Sekretarieti za Mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa ili kuwe na ufanisi na ubora wenye tija katika utekelezaji wa shughuli za maendeleo hasa katika usimamizi wa miradi na utoaji wa huduma bora kwa wananchi.

Amesema suala la utoaji wa mikopo ya asilimia 10 watendaji wanatoa huduma hizo lakini pia hawafuati kanuni zilizopo kwenye utoaji wa mikopo kama inavyotakiwa na Serikali.

“Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan wakati anatimiza miaka miwili alisema asilimia kubwa ya mikopo hii inayotolewa hua hairudi hivyo ni wajibu wa Wakurugenzi kusimamia mikopo”amesema Mhe. Mdee

Ameishauri Ofisi ya Rais- TAMISEMI kuongeza kigezo cha urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 ambapo Serikali iliweka dhamira njema ya kuwasaidia wananchi lakini inaonekana dhamira hiyo inatumiwa vibaya.

Aidha, Kamati imeishauri Ofisi ya Rais- TAMISEMI miongoni mwa vigezo vya kupima ustadi wa Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kiongezwe kigezo cha ufanisi wa Mkurugenzi katika kutoa mikopo na kufuatilia ipasavyo marejesho ya mikopo hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa imewataka Wakurugenzi hao kutambua kuwa wameaminiwa na Rais Samia ili kumsaidia kwa kufanya kazi kwa uadilifu, na uaminifu mkubwa.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa