• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

Halmashauri ya Manispaa ya Lindi yafanya kikao cha Robo ya kwanza 2024 cha MTAKUWWA.

Imetumwa: November 19th, 2024


Halmashauri ya Manispaa ya Lindi imefanya kikao cha Robo ya Kwanza cha Mpango Kazi wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili Dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) kwa mwaka 2024. Kikao hicho kimefanyika leo Novemba 19,2024 kwa kujadili hatua na mikakati ya kutokomeza ukatili katika jamii, na kujizatiti kwa kutekeleza majukumu ya kila mmoja katika kamati hiyo.

Mwenyekiti wa Kamati hiyo, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi, Juma Mnwele, aliwashauri wajumbe wa kamati hiyo kuendelea na juhudi zao katika kutokomeza ukatili kwa wanawake na watoto, akisisitiza kuwa nafasi za kila mmoja ni muhimu katika kufanikisha lengo hilo. "Nafasi zetu ni muhimu katika kamati hii katika kuisaidia jamii kuondokana na hali hii na tukishirikiana kwa pamoja tunaweza," alisema Mnwele.

Mchungaji Zakaria Lyakungi alieleza shukrani kwa serikali kwa kutambua umuhimu wa kuhusisha viongozi wa dini katika mapambano dhidi ya ukatili, akibainisha kwamba viongozi wa dini wana mchango mkubwa katika kujenga maadili bora katika jamii, na kwamba maadili mema ni nguzo muhimu ya kupambana na vitendo vya ukatili.

Naye, Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo, Consolata Singano, alikiri kuwepo kwa mashtaka ya ukatili wa kijinsia na dhidi ya wanawake na watoto, na kusema kwamba mahakama inawajibika kutoa haki kwa mujibu wa sheria na miongozo ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

MTAKUWWA ni kamati inayojumuisha wataalamu kutoka Halmashauri, ikiongozwa na Mkurugenzi wa Halmashauri, na katibu akiwa ni Afisa Ustawi wa Jamii. Wajumbe wa kamati hii ni pamoja na viongozi wa dini, afisa upelelezi, wazee maarufu, na wataalamu mbalimbali kutoka Halmashauri.

Kamati hii ina jukumu la kuimarisha mikakati ya kupambana na ukatili na kuhamasisha jamii kuondokana na vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto, kwa kushirikiana na wadau mbalimbali katika ngazi ya jamii, serikali, na vyombo vya sheria.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa