• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

FURSA ZA UWEKEZAJI KATIKA MANISPAA YA LINDI

Imetumwa: June 10th, 2020

Zijue fursa za uwekezaji zinazochangamkiwa na wawekezaji na wadau mbalimbali katika manispaa ya Lindi:

  • Ndipo unajengwa mtambo mkubwa wa kisasa wa uchakataji Gesi Asilia (LNG plant) wenye thamani ya USD 30Billion sawa na Tshs 70 Trillioni . mradi huu unatarajiwa kuwa wenye thamani zaidi kuwahi kutokea kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati. Utakuwa na uwezo wa kulisha viwanda vingine vingi vitakavyokuwa vikitumia by products zake. Jirani na eneo hili la LNG limetengwa eneo lenye ukubwa wa zaidi ya ekari 15,000 kwa ajili ya viwanda hivyo tarajiwa (Petro Chemical Industries). Kupitia uwekezaji huo, ajira nyingi zinatarajiwa kuzalishwa nchini. 

       


  • Ndio Manispaa inayojishughulisha na kilimo na ufugaji kwa kiwango kikubwa kuliko Manispaa zote nchini, hii inatokana na kuwa na eneo kubwa lenye Uoto mzuri na vyanzo vya kutosha vya Maji. Mwaka 2017/18 zaidi ya ekari 40,000 ziligawiwa kwa watu /taasisi mbalimbali kwa ajili ya Uwekezaji wa Kilimo cha Korosho na Ufuta.  Mazao haya kwasasa ndiyo yanaongoza kwa kuliingizia Taifa fedha za Kigeni. Maeneo bado yanaendelea kutolewa kwa watu na taasisi zenye mahitaji ya  uwekezaji.


Korosho

Ufuta


  • Pia ina eneo la fukwe lenye urefu wa zaidi ya kilometa 200 zinazosadikiwa kuwa miongoni mwa fukwe nzuri na bora kabisa duniani. Maeneo haya ambayo hayajatumika kikamilifu yanafaa kwa ajili ya shughuli za Kitalii, mapumziko, michezo na uvuvi. Kutokana na uwekezaji mkubwa wa kiwanda cha kuchakata Gesi Asilia (LNG) , ni dhahiri kuwa mahitaji ya huduma za hoteli na maeneo ya burudani fukweni yatakuwa makubwa. Tunakaribisha maombi ya uwekezaji katika eneo hili.


  • Halmashauri ina maeneo mengi yenye  akiba kubwa sana ya madini ya “Gypsum” na “graphite”. Uwepo wa madini haya muhimu kwa matumizi ya viwandani, yanathibitisha kuwa Lindi ndio sehemu sahihi ya uwekezaji kwa taasisi na mwanachi mmoja mmoja.


  • Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) ni miongoni mwa taasisi zilizoweza kubaini “potentials” zilizopo Manispaa ya Lindi na sasa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kipo hatua nzuri ya uanzishaji wa Ndaki ya Kilimo na Teknolojia ya Uvuvi (College of Agriculture and Fisheries Technology) eneo la Ngongo, aidha Chuo cha Taifa cha Usafirishaji nao wapo hatua nzuri wa Uanzishaji wa Ndaki ya Usafirshaji  Majini na masuala ya Mafuta (Maritime studies and Petroleum Technology eneo la Kikwetu).


The College of Agriculture and Fisheries Technology (UDSM) eneo la NgongoThe College of Agriculture and Fisheries Technology (UDSM) eneo la Ngongo

The College of Maritime studies and Petroleum Technology (NIT) eneo la Kikwetu


  • Kwa asiyefahamu, Manispaa ya lindi ndiyo Manispaa iliyo karibu zaidi na jiji la Dar_es_salaam, baada ya Manispaa ya Morogoro. Ni kwababu hiyo tunadhani kuna kila sababu ya watu na taasisi mbalimbali kuchangamkia fursa zilizopo ikiwa ni pamoja na kununua viwanja vya KIKWETU na NGONGO.


Viwanja vinauzwa kwa bei rafiki  kama ifuatavyo:




Na
MATUMIZI YA ARDHI

BEI YA KWA KILA MITA YA MRABA

1

Makazi

2,500/=

2

Makazi na biashara

3,000/=

3

Majengo ya umma (public building) taasisi, zahanati, huduma za ibada (religious institution), taasisi za elimu, shule.

2,500/=

4

Biashara, Hoteli, Taasisi binafsi, Housing Estate

4,500/=


  • Baada ya kuongezewa jimbo la Mchinga, kwasasa Manispaa ya Lindi inadhaniwa kuwa ndio Manispaa yenye eneo kubwa zaidi la utawala kuliko Manispaa zote nchini kwani inakadiriwa kuwa na eneo lenye ukubwa wa kilometa za mraba zaidi ya 3900. Kwa mjibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, majimbo yote mawili yalikuwa na jumla ya wakazi takribani 142,142 na hivyo kuwa miongoni mwa Halmashauri zenye idadi ndogo zaidi ya wakazi.  Hapa chini ni mlinganisho wa Manispaa ya Lindi na baadhi ya Halmashauri ya Manispaa nyingine kwa ukubwa wa eneo na idadi ya wakazi.

Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa