• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Barua Pepe |
    • Malalamiko |
Lindi Municipal Council
Lindi Municipal Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Maadili ya Msingi
    • mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu
      • Idara ya Elimu ya Awali na Elimu Msingi
      • Idara ya Elimu ya Sekondari
      • Idara ya Mipango na Uratibu
      • Idara ya Huduma za Afya,Lishe na Ustawi wa Jamii
      • Idara ya Biashara,Viwanda na Uwekezaji
      • Idara ya Kilimo,Mifugo na Uvuvi
      • Idara ya Ujenzi na Maendeleo ya Miundombinu Vijijini na Mjini
      • Idara ya Maendeleo ya jamii
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha TEHAMA na Takwimu
      • Kitengo cha Ukaguzi wa Ndani
      • Kitengo cha Udhibiti wa Taka Ngumu na Usafi wa Mazingira
      • Kitengo cha Ununuzi
      • Kitengo cha Fedha na Uhasibu
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
      • Kitengo cha Michezo, Utamaduni na Sanaa
      • Kitengo cha Maliasili na Uhifadhi wa Mazingira
  • Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Mtandao wa Barabara
    • Maliasili
  • Huduma zetu
    • Huduma za Elimu
    • Huduma za Afya
    • Huduma ya Maji
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipangomiji na Maliasili
      • Ujenzi, Uchumi na Mazingira
      • Fedha, Uongozi na Mipango
      • Kudhibiti Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba za vikao
    • Ratiba ya kuonana na Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyokamilika
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi itakayotekelezwa
  • Machapisho
    • Sheria
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo
    • Taratibu
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Picha
    • Hotuba
    • Habari
    • Matukio
    • Joining instructions forms
  • E-Learning
    • past papers
    • Notes

Kata ya Mtanda

UTANGULIZI

Kata ya mtanda ni miongoni mwa kata 20 zilizopo katika Manispaa ya Lindi.Ina wakazi wapatao 5683, kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2012, ambapo kati yao wanaume walikuwa ni 2743 na wanawake 2940. Kwa sasa inakadiliwa kuwa na ongezeko la watu wasiopungua 1560.

UONGOZI WA UTAWALA;

Kata ya Mtanda ina jumla ya mitaa 7 ambayo ni Mtandakati, Mtanda juu, Mtanda kaliakoo kwa upande wa mjini na upande kanda B yani Kineng`ene kuna mitaa ya Mmukule, Mchochoro, Nanembo na Mtutu.

WATUMISHI NGAZI YA KATA.

Kata ya Mtanda ina Mtendaji wa kata na watendaji wa Mitaa wanne, kata inayo Afisa wa Afya, Maendeleo ya jamii, mratibu Elimu kata, Afisa kilimo na Afisa wa mifugo.Wapo pia wahudumu wa afya katika Zahanati ya Kineng`ene wapatao sita (6) kati yao wanaume ni wanne(4) na wanawake wawili (2).

UPUNGUFU;

Kata ya Mtanda ina upungufu wa watendaji wa Mitaa watatu(3), walimu wa shule za msingi kumi na tano (15) na (10) kwa shule za sekondari. Yaani Lindi na kineng`ene sekondari.

MIRADI YA MAENDELEO;

Kama ilivoripotiwa kwenye taarifa za robo ya tatu na ya nne 2018/2019 ya hadi robo ya kwanza 2019/2020 kuwa miradi ya maendeleo ambayo ilikuwa inashughulikiwa ni ile ya ujenzi wa kituo cha Afya kineng`ene ambao tayri ulishakamilika kwa karibu asilimia 98/99, na kwa sasa kusubiriwa vifaa tiba na Wataalam ambapo Serikali yenyewe ndio itawajibika katika upatikanaji wake.

BARAZA LA KATA;

Baraza la Ardhi la kata ya Mtanda kwa kipindi hiki cha robo ya Pili (Oktoba-Disemba) 2019/2020, katika Mitaa yote ya kata hii hakujapokelewa mashauri/malalamiko yoyote yale yaliyopokelewa.

HALI YA KATA;

Hali ya maendeleo katika kata inaendelea vizuri kwani uboreshwaji wa mahusiano katika ngazi ya jamii na miradi mbalimbali ya maendeleo umeimalika na wanajamii kuongeza hali ya kujitolea katika miradi yao badala ya dhana yakuona Serikali ndio yenye jukumu la kujenga, kusimamia na kuilinda miradi yao ata inapokuwa imekamilika.

Kwa sasa wameelimishwa na wanajitoa katika kushiriki hatua zote za miradi na shughuli mbalimbali za maendeleo inayofanyika katika maeneo yao.

ELIMU/HALI YA UFAULU;

Kata ya Mtanda ina shule nne kati yake mbili ni za msingi na mbili ni za sekondari ambazo zimegawanyika kwa jiografia ya Kata hii, nazo ni kama zifuatazo;

1.Shule ya msingi Mtanda, na shule ya sekondari Lindi zipo kanda A, na kwa kanda B, kuna shule ya msingi kineng`ene na shule ya sekondari kineng`ene. Katika cha robo ya pili shule hizo mbili za msingi wanafunzi  waliohitimu darasa la saba jumla yao ni mia moja na kumi na tatu (113) kwa mchanganuo ufuatao;

i.Shule ya msingi Mtanda wavulana 20 na wasichana 32 jumla 52 na wote wamefaulu na wanatarajia kujiunga kidato cha kwanza.

ii.Shule ya msingi Kineng`ene wavulana 26 na wasichana 35. Matokeo ya mtihani wa darasa la saba wavulana 25 waliweza kufaulu na mmoja alifeli na wasichana 34 waliweza kufaulu na mmoja tu ndiye aliyefeli hivyo kufanya jumla ya wanafunzi 59 kufaulu na wanatarajia kujiunga na kidato cha kwanza ifikapo mwaka 2020.

Hivyo kata ya Mtanda imefanikiwa kufaulisha wanafunzi mia moja na kumi na mmoja (111) kati ya wanafunzi mia moja kumi na tatu (113) .

HALI YA MAHUDHURIO YA WANAFUNZI (UTORO);

Kwa kipindi cha robo hii ya pili ya Ofisi ya kata ya Mtanda haijapokea malalamiko ya utoro ambao kwa shule zake zote yani za msingi na sekondari wala tatizo la ujauzito kwa mwanafunzi yeyote.

HALI YA UFUNDISHAJI;

Kwa kipindi hiki cha robo ya pili hali ya ufundishaji katika shule za kata za kata hii umeendelea kuwa mzuri, Ofisi haijapokea malalamiko kuhusu ufundishwaji hafifu kwa wanafunzi wa shule yoyote ile, pongezi za dhati zimetolewa kwa kazi nzuri iliyofanywa na walimu kwa ufundishaji ambao umeleta ufaulu mkubwa katika shule zote mbili za msingi za kata hii kama ilivyoelezwa kwenye kipengele husika hapo juu.

UDHIBITI UBORA NA URATIBU;

Hali ya ukaguzi na uratibu kwa kipindi cha robo ya pili 2019/2020 katika kata hii zoezi wataalam hao waliweza kutembelea mara moja katika shule za kata hii.

HALI YA MAGONJWA YA MILIPUKO, NJAA, UHALIFU NA VIFO.

Kwa kipindi cha pili 2019/2020, ni kama kwa robo ya kwanza kata ya Mtanda hakujitokeza maafa, milipuko, njaa, changamoto ilijitokeza na kuathiri shughuli Afya za wakazi au shughuli za kiuchumi.

HALI YA MAJANGA;

Hakuna janga lolote lililojitokeza katika kipindi cha robo hii ya pili 2019/2020, kwa ujumla hali ni shwari kwa wakazi wa kata ya Mtanda na mali zao na wanaendelea kufanya shughuli zao mbalimbali zinazowaletea maendeleo.

MAENDELEO YA KILIMO, UVUVI NA MIFUGO.

Katika kata ya Mtanda wapo baadhi ya wananchi ambao wanajishughulisha na kilimo ufugaji mdogomdogo wa aina mbalimbali za mifugo kwa lengo la kujiongezea kipato na pia kama sehemu yao ya maisha.

Wafugaji na wakulima hao hupata ushauri kwa wataalam waliopo katika ngazi ya kata hii.

Kwa sasa kata inakadiliwa kuwa na mifugo kwa idadi ifuatayo hapa chini.

  • Ng`ombe 238
  • Kondoo 56
  • Kanga 69
  • Mbwa 131
  • Bata 459
  • Mbuzi 681
  • Kuku 43,714
  • Nguruwe 115
  • Bata mzinga 27.

Hivyo kufanya idadi ya mifugo hiyo kuwa 45,490.

Kadhalika, katika Kata ya Mtanda wapo pia wakazi ambao wanajishughulisha na kilimo cha bustani za mbogamboga na kilimo cha mazao ya chakula na biashara kwa ajili ya matumizi yao ya kawaida.

Kata ya Mtanda kama zilivyo kata nyingine ambazo baadhi ya wakazi wake wanapenda kujiunga na shughuli za kiushiriki kata kuwa haina chama chake cha msingi kinachojitegemea, hivyo wakulima wake wameunganika na wakulima wa maeneo mengine na kuwa wanachama cha KITUMIKI, ambapo kwa umoja wao uuza mazao na kupata pembejeo zao kupitia chama hicho.

UIMALISHAJI WA DHANA YA UZALENDO NA UTAIFA.

Kuhusu uimalishaji wa dhana ya uzalendo na utaifa vijana wanaendelea kuhamasishwa kuwa wazalendo katika kulinda rasilimali za nchi kulinda miradi mbalimbali ya maendeleo iliyopo katika kata, pia kutoa taarifa za waharifa wa miradi ya maendeleo na mali za mtu mmoja mmoja ili kuhakikisha usalama wa watu na mali zao katika kata ya Mtanda zinakuwa salama salimini.

Aidha kwa sasa kata iliweza kuandikisha vijana na kujiunga katika mafunzo ya mgambo (Jeshi la Akiba) vijana hao sambamba na vijana wengine wa Manispaa ya Lindi wanaweza kuhitimu mafunzo hayo katika kipindi cha robo hii ya pili panapo tarehe 20/12/2019.

Kata ya Mtanda haikubaki kama eneo lakufanyia mafunzo tu kama inavyokuwa kuwa kwa maeneo mengine bali ilihakikisha inatoa na vijana wa kushiriki mafunzo hayo.

HALI YA USAFI WA MAZINGIRA;

Kama ilivyoadakwa Kata ya Mtanda, sawa na kata nyingine za Manispaa ya Lindi katika utekelezaji wa agizo la Mhe,Raisi wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kuhusu usafi wa mazingira kwa kila jumamosi ya kila mwisho wa mwezi kwenye maeneo mbalimbali ya Umma/Taasisi zilizopo katika kata hii.

Aidha bado kata inaendelea na utaratibu wake iliyojiwekea wa kufanya usafi na jumamosi zingine pale itakapobaini kuna ulazima wa kufanya usafi eneo lolote.

Changamoto kubwa ni kukosa chombo cha usafiri wa kuzolea taka hizo pale zinapokuwa zimekusanywa, hivyo kuwa kero zinapokuwa hazijazolewa kwa muda mrefu na zikiwa katika maeneo ya makazi ya watu.

UKUSANYAJI WA TAKA NGUMU;

Katika zoezi hili ukusanyaji wa taka ngumu, kata ya Mtanda inaendelea kuiomba Halmashauri ya Manispaa ya Lindi kuendelea kuboresha katika eneo hili pamoja na changamoto kubwa ya fedha iliyonayo, kwakuweza kupeleka lori walau mara moja kwa wiki katika eneo la Mtanda ili kupunguza kero hiyo ambayo imelalamikiwa kwa muda mrefu kwani wananchi wa Mtanda hao ni sehemu ya wakazi wa Manispaa ya Lindi hivyo nao wapewe kipaumbele katika kupatiwa huduma hiyo.

MAENDELEO YA JAMII;

Hadi taarifa hii inaandaliwa ya kipindi cha robo ya pili 2019/2020, kata ya Mtanda imeendelea kuwa na takribani ya vikundi visivyopungua 26 vya vijana na wanawake (wajasiliamali) ambavyo vina usajiri halali kwa Halmashauri ya Manispaa ya Lindi.Kwa kipindi cha robo hii ya kwanza 2019/2020, hakuna kikundi chochote ambacho kimeweza kuwezeshwa na Halmashauri kwa namna yoyote ile.

TAARIFA ZA TASAF.

Kata hii ni miongoni mwa kata ambazo zinapata uwezeshwaji wa kifedha za ruzuku ya kaya masikini katika Mtaa wake wa Mtanda Juu, lakini tangu kipindi cha robo hii ya pili haijapokea fedha kiasi chochote ile, isipokuwa walipatiwa mafunzo maalum kiujasiliamali na hatua za kiutekelezaji zinaendelea vizuri.

Hivyo ni matumaini ya kata yetu kuwa mara watakapoanza kuwezeshwa kwa awamu hiyo walengwa hao watakuwa wamepunguza kiasi kikubwa cha umasikini kama sio kuondokana nao kabisa.

TAARIFA YA KUFANYIKA KWA UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA.

Kata ya Mtanda kama ilivyokuwa kwa kata nyingine za Tanzania iliweza kushiriki katika zoezi zima la uchaguzi wa viongozi wa Serikali za mitaa katika mitaa yake yote saba (7). Mchakato huo kwa ujumla wake ulifanyika kwa amani na utulivu katika mitaa yake yote na hatimaye kuweza kuwapata viongozi wake wote kutoka katika Chama Tawala yani Chama cha Mapinduzi, tayari viongozi hao walishaapiwa na wameanza kutekeleza majukumu yao katika maeneo yao.

CHANGAMOTO;

Kwa kipindi cha robo hii ya pili changamoto ambazo zimeendelea kuwapa zile ambazo pia ziliripotiwa nazo ni kama zifuatazo;

  • Ukamilishaji wa nyumba ya mwalimu katika shule ya msingi Mtanda ambayo mpaka sasa ina takribani miaka isiyopungua kumi na mbili tangu kuanza kwa ujenzi wake kama ilivyoripotiwa katika taarifa ya robo ya kwanza.
  • Ukosefu wamiundombinu katika nyumba tatu za walimu wa shule ya msingi kineng`ene.

MAFANIKIO;

Kama ilivyoada kila penye changamoto pia mafanikio hayakosekani, yapo baadhi ya mafanikio yalipatikana katika kata ya Mtanda kutokana na ushirikiano wa wanajamii, uongozi wa kata pamoja na wadau mbalimbali wapenda maendeleo katika kata hii nayo ni kama yafuatayo;

  • Kukamilika kwa upanuzi wa Zahanati ya kineng`ene na kuwa kituo cha Afya cha kisasa kilichosalia kwa sasa ni kupatiwa vifaa tiba na Wataalam tu msisitizo unaendelea kutolewa na wananchi ni kuiomba Serikali kuangalia uwezekano wa kupeleka mahitaji husika ili wananchi wafaidike na matunda yao na ya Serikali yao.
  • Kama iliripotiwa katika Taarifa ya robo ya kwanza kuwa, Ukarabati wa vyoo vya walimu shule ya msingi Mtanda ambapo ilikuwa ni changamoto ya muda mrefu, Uongozi wa kata na shule ulijipanga na kukubaliana kufanya harambee siku ya mahafari ya shule hiyo na kufanikiwa kukusanya kiasi cha fedha na vifaa hatimaye vyoo hivyo sasa vimekarabatiwa na vinatumika pasipo kusubiri fedha toka Halmashauri/ Serikali kuu.
  • Kuimalika kwa hali ya Ulinzi na Usalama kwani matukio mbalimbali ya uhalifu yalianza kuiandama kata ya Mtanda.


Matangazo

  • THE PROVISION OF CONSTRUCTION SUPERVISION CONSULTANCY SERVICES FOR URBAN INFRASTRUCTURE DEVELOPMENT IN LINDI MUNICIPALITY UNDER THE TACTIC PROJECT March 09, 2025
  • KUONGEZA KWA MUDA WA RUFAA November 13, 2024
  • TAARIFA KWA UMMA October 31, 2024
  • MAJINA YA WALIOITWA KWENYE USAILI October 01, 2024
  • Ona Yote

Habari Mpya

  • SPORTS DEVELOPMENT AID YAKABIDHI MIPIRA 585 YENYE THAMANI YA SHILINGI MILIONI 35 MKOA WA LINDI.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • KATIBU TAWALA MKOA WA LINDI AWAPONGEZA WAKAZI WA MANISPAA YA LINDI KWA KUJITOKEZA KWENYE MAZOEZI YA MUUNGANO DAY.

    April 26, 2025
  • WATUMISHI MANISPAA YA LINDI WAJENGEWA UELEWA JUU YA MASUALA YA RUSHWA.

    April 08, 2025
  • Ona Yote

Video

NENO LA DC MWANZIVA KWENYE SIKU YA WANAWAKE DUNIANI HALMASHAURI YA MANISPAA LINDI
Video Zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Zabuni
  • sheria mbalimbali
  • Ratiba za vikao
  • Orodha ya Madiwani
  • Mikakati ya Halmashauri
  • Historia ya Manispaa ya Lindi
  • Miradi inayoendelea
  • Mfumo wa Vibali vya Safari Nje ya Nchi

Tovuti Linganifu

  • Ikulu
  • OR - TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Idara Kuu ya Takwimu (NBS)
  • Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Idadi ya Watembeleaji Duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

writingMasterThesis

Ramani

Wasiliana Nasi

    Mkurugenzi wa Manispaa

    Anuani ya Posta: 1070 Lindi

    Simu: +255232202164

    Simu ya mkononi: +255717469888

    Barua Pepe: info@lindimc.go.tz

Anwani Nyingine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Vigezo na Masharti
    • Ramani ya Tovuti

Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa