Mkuu wa Mkoa wa Lindi Mheshimiwa Godfrey Zambi afanya ziara ya kutembelea shule za msingi na sekondari Manispaa ya Lindi ambapo amewataka Watendaji Kata husika kuhakikisha wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza wanaripoti wote,Pia amewataka Mkuu wa Wilaya na watendaji wake kujenga madarasa,vyoo,viti na meza na miundombinu yote muhimu katika shule zenye changamoto hizo ili kuhakikisha wanafunzi wanasoma vizuri.Pia kufanya msawazo wa walimu kutoka kwenye shule zenye walimu wengi kwenda kwenye shule zenye walimu wachache ameagiza zoezi hilo litekelezwe ndani ya miezi mitatu ametoa agizo hilo akiwa katika shule ya sekondari Mingoyo ikiwa ni miongoni mwa shule alizotembelea.Mkuu wa mkoa aahidi mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya ukarabati wa shule ya msingi Msinjahili na Mkuu wa Wilaya aahidi bati 40 geji 30 kwa ajili ya ukarabati huo pia.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa