Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa Meja Jenerali IM Mhona ametembelea Manispaa ya Lindi akiwa na baadhi ya washiriki katika ziara ya mafunzo kwa vitendo ikiwa na lengo na dhumuni la kujifunza kwa undani kuhusu Mkoa wa Lindi. Meja Jenerali amewapongeza viongozi wa Manispaa kwa mikakati na malengo mazuri yanayohakikisha maendeleo ya Manispaa na Mkoa kwa ujumla.
Meja Jenerali na washiriki wa mafunzo wa chuo cha Ulinzi walipata nafasi ya kutembelea baadhi ya maeneo katika Manispaa. Miongoni mwa maeneo waliyotembelea ni pamoja na Uwanja wa ndege (Kikwetu), Shule ya sekondari Lindi kuangalia ukarabati uliofanyika katika shule hiyo ambapo Meja Jenerali ameahidi kutoa kiasi cha fedha shilingi Millioni moja ili kusaidia utengenezaji wa viti na meza vya wanafunzi.
Pia walipata nafasi ya kutembelea Kituo cha Afya Mnazimmoja ambapo Mkuu wa Chuo ameupongeza uongozi wa Kituo kwa maendeleo makubwa waliyoyafikia hasa kwa huduma nzuri wanazozitoa.
Vile vile alipata wasaa wa kutembelea Kikundi cha vijana cha Mitema ambapo aliwapongeza vijana hao kwa kazi nzuri wanayoifanya na aliwachangia kiasi cha pesa shilingi laki tano ili kiwasaidie kutatua changamoto ndogo ndogo zinazowakabili.
Meja Jenerali akimsalimia mzazi wodi ya akina mama waliojifungua alipotembelea kituo cha Afya Mnazimmoja.
Mkuu wa Chuo cha Ulinzi cha Taifa alipotembelea shule ya sekondari Lindi.
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa