Mkurugenzi wa Manispaa wa Manispaa ya Lindi anawatangazia Wananchi wote kuwa Tarehe 29.06.2020 siku ya Jumatatu kuwa shule zote za Msingi na Sekondari zitafunguliwa Rasmi Kufuatia Tamko la MHE: RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI alilotoa BUNGENI wakati akivunja BUNGE LA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA tarehe 16.06.2020 hii ni kutokana na kupungua kwa kiasi kikubwa cha maambukizi ya UGONJWA wa COVID - 19 (VIRUSI VYA CORONA). Sule hizo zilifungwa TAREHE 17.03.2020 kwa ajili ya kuchukua tahadhari ya Maambukizi ya Virusi vya CORONA.
Hivyo Wazazi wote wanatakiwa Kuhakikisha kuwa Wanafunzi wote wanaandaliwa na Kuripoti Shuleni Bila Kukosa Masomo Yataanza Rasmi Tarehe 29.06.2020
Bofya CHINI kupata Tangazo katika Mfumo wa PDF ↓↓↓↓↓
Municipal Director
Anuani ya Posta: 1070 Lindi
Simu: +255232202164
Simu ya mkononi: +255767042958
Barua Pepe: info@lindimc.go.tz
Hakimiliki @2020 Manispaa ya Lindi. Haki zote zimehifadhiwa